Posts

Sababu za Serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina kufuata muelekeo sawa na wa utawala wa Kizayuni dhidi ya HAMAS

Image
  Serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina imeendelea kufuata muelekeo sawa na wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS kwa kutoa amri ya kufungwa Chaneli ya Televisheni ya Al Jazeera ya Qatar huko Ramallah. Siku ya Jumatano usiku, Mamlaka ya Ndani ya Palestina ilitangaza kuwa imepiga marufuku shughuli za Al Jazeera kwa sababu ya ilichokiita "kukiuka sheria na kanuni za ndani na kutangaza maudhui za kichochezi". Kutokana na uamuzi huo, shughuli zote za ofisi ya Al Jazeera ndani ya Palestina, ikiwa ni pamoja na utangazaji wa vipindi na shughuli za wanahabari na maripota wa chaneli hiyo zimesimamishwa. Ofisi ya Al Jazeera, Ramallah, Ukingo wa Magharibi Hatua hiyo iliyochukuliwa na Mamlaka ya Ndani ya Palestina inaweza kuchambuliwa kwa kuzingatia nukta kadhaa. Kwanza ni kuwa, hatua hiyo imechukuliwa...

Utawala wa Kizayuni wakiri kuuliwa wanajeshi wake zaidi ya 800 na kujiuwa wengine 28

Image
  Ikiwa imepita siku 456 tangu Israel ianzishe vita dhidi ya Gaza, utawala huo umekiri kuhusu baadhi ya maafa na vipigo ulivyopata tangu kutekelezwa Oparesheni ya Kimbunga cha al Aqsa na wanamuqawama wa Palestina. Jeshi la utawala wa Kizayuni limetangaza katika taarifa yake kuwa wanajeshi wake zaidi ya 800 wameangamizwa vitani huko Gaza tangu kuanza vita dhidi ya eneo hilo Oktoba 7 mwaka 2023.  Ripoti ya Israel imeeleza kuwa, wanajeshi 329 wa utawala huo waliuawa wakati wa operesheni hiyo ya Oktoba 7, na wengine 390 waliuawa wakati wa operesheni ya ardhini huko Gaza.  Jeshi la utawala wa Kizayuni pia limekiri kuwa wanajeshi wake 50 waliangamizwa katika oparesheni ya nchi kavu huko Lebanon.  Kwa mujibu wa tangazo la jeshi la utawala wa Kizayuni, katika kipindi kilichotajwa, askari 28 wa utawala huo wakiwemo askari 16 wa kikosi cha akiba wamejiua; na Wazayuni 11 pia waliuawa katika ope...

Biden kutuma shehena ya silaha kwa Israel

Image
  Chanzo cha picha, EPA Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imearifu Bunge la Congress kuhusu mpango wa kuiuzia Israel silaha kwa thamani ya $8bn (£6.4bn), afisa wa Marekani ameithibitishia BBC. Shehena ya silaha, ambayo inahitaji idhini kutoka kwa kamati za Bunge na Seneti, inajumuisha makombora na silaha nyingine. Hatua hiyo inajiri takribani wiki mbili kabla ya Rais Joe Biden kuondoka madarakani. Washington imekataa wito wa kusitisha msaada wa kijeshi kwa Israel kwa sababu ya idadi ya raia waliouawa wakati wa vita huko Gaza. Mwezi Agosti, Marekani iliidhinisha uuzaji wa ndege za kivita zenye thamani ya $20bn na vifaa vingine vya kijeshi kwa Israel. Mpango wa Shehena ya hivi karibuni ina makombora ya kutoka angani na mabomu, afisa huyo wa Marekani alisema. Chanzo kimoja kinachofahamu mauzo hayo kiliiambia BBC siku ya Jumamosi: "Rais ameweka wazi kuwa Israel ina haki ya kutetea raia wake, kwa kuzingatia sheria za kimataifa za kibinadamu, na kuzuia uchokozi kutoka kwa Iran...

Vikosi vya Guatemala vyawasili Haiti kupambana na magenge ya uhalifu

Image
  Chanzo cha picha, Reuters Kikosi cha wanajeshi 150 wa Guatemala kimewasili Haiti, kikiwa na jukumu la kusaidia kurejesha utulivu huku kukiwa na machafuko yanayotekelezwa na magenge yenye silaha. Kundi la kwanza la wanajeshi 75 liliwasili siku ya Ijumaa na wengine 75 Jumamosi, wote wakiwa wamesajiliwa kutoka Wizara ya polisi wa kijeshi, kulingana na serikali ya Guatemala. Hali ya hatari imekuwa ikitanda katika taifa hilo la Caribean kwa miezi kadhaa huku serikali ikipambana na magenge ya kikatili ambayo yamedhibiti sehemu kubwa ya mji mkuu wa Port-au-Prince. Vikosi hivyo viko nchini Haiti ili kuimarisha kikosi cha usalama kinachoungwa mkono na Umoja wa Mataifa kinachoongozwa na Kenya ambacho hadi sasa kimeshindwa kuzuia ghasia. Kenya ilituma karibu maafisa 400 wa polisi mwezi Juni na Julai mwaka jana kusaidia kupambana na magenge hayo. Hiki kilikuwa ni awamu ya kwanza ya kikosi cha kimataifa kilichoidhinishwa na Umoja wa Mataifa ambacho kitaundwa na maafisa 2,500 kut...

Man Utd 'wana wasiwasi sana, wanaogopa sana' – Amorim

Image
  Chanzo cha picha, Reuters Maelezo ya picha, Manchester United haijashinda mchezo wowote kati ya nane iliyopita -ligi ya ugenini dhidi ya Liverpool - sare nne na kupoteza mara nne Kocha wa Manchester United, Ruben Amorim anasema wachezaji wake "wana wasiwasi sana, wanaogopa sana" na kwamba mwenendo mbaya wa timu yake umemletea madhara. United itawakabili vinara Liverpool siku ya Jumapili (16:30 GMT) baada ya kushindwa mara nne mfululizo katika michuano yote - ikiwa ni pamoja na tatu katika Ligi ya mabingwa. Wameshinda mechi mbili pekee za ligi kuu tangu Amorim achukue usukani mwezi Novemba na kupata alama saba pekee. “Unaweza kuniona usoni mwangu, unaweza kulinganisha kipindi nilipowasili na sasa,” alisema Amorim, ambaye amepoteza mechi tano kati ya nane za Ligi Kuu England. "Bila shaka kuna shinikizo nyingi. Kwangu mimi, ni fahari na pia kupata matokeo mazuri. "Ni vigumu zaidi wakati hatufanyi vizuri." United ilifungwa 3-0 nyumbani na Bournemouth, 2-0 na Wo...

Ripoti Maalum: Je, Urusi inaweza kutoa nini kwa utawala mpya nchini Syria?

Image
  4 Januari 2025 "Uhalifu wa Urusi hapa hauelezeki," alisema Ahmed Taha, kamanda mkuu wa waasi katika mji wa Douma, maili sita kaskazini mashariki mwa Damascus. "Ilikuwa uhalifu wa kiwango kisichoweza kuelezeka." Alisema haya alipokuwa kwenye mtaa wa jangwa ambao umejengwa majengo ya makazi mengi ambayo yalikuwa yameporomoka na kuwa vifusi. Hapo awali Douma ilikuwa mahali penye ustawi, ikiwa mji mkuu wa eneo linalojulikana kama "kapu la mkate wa Damascus," lakini sasa sehemu kubwa imeharibiwa baada ya mapigano makali wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Syria vilivyodumu miaka 14. Makazi na shule pia viligeuka kuwa vifusi, na... Matangazo "Kabla ya vita, Taha alikuwa mkandarasi na mfanyabiashara. Lakini aliamua kuchukua silaha mwaka 2011 baada ya utawala wa Syria kukandamiza maandamano ya amani huko Douma kwa ukatili, na akawa mmoja wa viongozi wa upinzani wenye silaha katika mji huo. Wakati muungano wa Kiislamu uliokuwa ukijulikan...

Wachunguzi wa Korea Kusini wamtaka kaimu rais arahisishe kukamatwa kwa Rais Yoon

Image
  Chanzo cha picha, Reuters/Tyrone Siu Maelezo ya picha, Polisi wakijaribu kuwazuia watu wakati wa maandamano ya kumpinga Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol, karibu na makazi yake rasmi huko Seoul, Korea Kusini, 4, Januari 2025. Wachunguzi wa Korea Kusini wamemtaka tena kaimu rais wa nchi hiyo Jumamosi kuamuru idara ya usalama ya rais kufuata agizo la kukamatwa kwa Rais aliyeondolewa madarakani Yoon Suk Yeol. Siku ya Ijumaa Idara ya usalama, pamoja na wanajeshi, waliwazuia waendesha mashtaka kumkamata Yoon Suk Yeol katika mzozo uliodumu kwa saa sita ndani ya makazi ya Yoon. Wachunguzi walipata hati ya kumkamata Yoon kutokana na tamko lake la muda mfupi la sheria ya kijeshi mwezi uliopita. Ofisi ya Uchunguzi wa Ufisadi kwa Maafisa wa Vyeo vya Juu, ambayo inachunguza kesi hiyo, ilisema Jumamosi ilimtaka tena kaimu Rais Choi Sang-mok, waziri wa fedha wa taifa hilo, kuamuru idara ya usalama ya rais kuonyesha ushirikiano na agizo la kibali hicho. Msemaji wa wizara ya...