Haniya: HAMAS haitasalimu amri, itaendeleza muqawama
Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kundi hilo la muqawama katu halitasalimu amri, bali litaendeleza mapambano yake kwa nguvu zote. Ismail Haniya amesema hayo katika taarifa, akijibu operesheni ya umwagaji damu iliyofanywa na wanajeshi makatili wa Israel dhidi ya kambi ya wakimbiizi ya Nuseirat, katikati mwa Ukanda wa Gaza na kuongeza kuwa: Hatutakata tamaa, tutaendelea kupigania haki zetu za msingi mkabala wa adui mtenda jinai. Wapalestina wasiopungua 210 waliuliwa shahidi na wengine zaidi ya 400 walijeruhiwa juzi Jumamosi katika mashambulizi ya kinyama ya anga ya Israel yaliyolenga kambi ya wakimbizi ya Nuseirat, maeneo ya mashariki ya Deir al-Balah, na kambi za al-Bureij na al-Maghazi katikati mwa Gaza, sanjari na uvamizi wa ghafla uliofanywa na magari mashariki na kaskazini magharibi mwa Nuseirat. Jinai za Wazayuni katika kambi y...