HAMAS na Jihadul-Islami zakabidhi rasmi majibu yao kwa mpango wa kusimamisha vita Ghaza
Harakati kuu za Muqawama na ukombozi wa Palestina za HAMAS na Jihadul-Islami zimetoa jibu rasmi kwa pendekezo linaloungwa mkono na Marekani la kusitisha mapigano Ghaza na kubadilishana mateka kwa wafungwa kwa kuongeza baadhi ya "maoni" kuhusu mpango huo. Hayo yamethibitishwa na wapatanishi wa Qatar na Misri. Katika taarifa ya pamoja ziliyotoa jana Jumanne, Hamas na Jihadul-Islami zimesisitiza kuwa ziko tayari kuzungumzia kwa mtazamo chanya mpango huo na kufikia makubaliano na kwamba kipaumbele chao ni "kusimamishwa kikamilifu" mashambulizi yanayoendelea ya Israel dhidi ya Ghaza. Afisa mwandamizi wa Hamas Osama Hamdan ameiambia kanali ya televisheni ya Al-Mayadeen ya Lebanon kwamba harakati yao "imewasilisha baadhi ya maoni kuhusu pendekezo hilo kwa wapatanishi". Hamdan amefafanua kuwa majibu ya Hamas yametilia mkazo msimamo kwamba makubaliano yoyote lazima yakomeshe uchokozi wa Wazayuni dhidi ya Wapalestina, yahaki...