Posts

Abdul Malik al Houthi: Saudia imeondoa aya za Qur'ani katika vitabu vya kiada ili kuwaridhisha Wazayuni

Image
  Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amewatuhumu viongozi wa Saudi Arabia kuwa wameondoa baadhi ya mafundisho ya Qur'ani katika progamu za kufundishia mashuleni ili kuwaridhisha Wazayuni. Abdul Malik al Houthi amesema kuwa utawala wa Saudi Arabia umeondoa aya za Qur'ani katika vitabu vya mtaala mashuleni (Syllabus) ili kuepuka kuwakasirisha Wazayuni. Amesema, aya hizo zinazochujwa na Saudia mashuleni ni zile zinazozungumzia jinai zilizotendwa na Wayahudi.   Qur'ani Tukufu  Afisa huyo wa Yemen ameongeza kuwa utawala wa Saudi Arabia hata umeondoa kikamilifu au baadhi ya sejemu za  suna za Mtume  Muhammad (s.a.w) katika programu za kielimu mashuleni na kusema kuwa hatua hiyo ya Saudia ni dhulma kwa vizazi vijavyo.  Al Houthi ameongeza kuwa Saudia imefanya hivi sambamba na mpango wake wa kuhuisha  uhusiano na utawala wa Kizayuni.  Umoja wa Falme za Kiarabu pia umefuata mkond

Msaada wa kijeshi wenye thamani ya dola bilioni 26 wa Marekani kwa Israel sambamba na vita vya Gaza

Image
  Baada ya mabishano na mvutano kati ya Wademokrat na Warepublican na Hitilafu za pande hizo mbili juu ya msaada wa kigeni, Baraza la Wawakilishi la Marekani limeidhinisha kifurushi cha msaada wa dola bilioni 60 kwa Ukraine na kifurushi kiingine cha dola bilioni 26 kama msaada wa kijeshi kwa Israel kwa kura 366 dhidi ya 58. Muswada huu lazima uidhinishwe na Seneti na kisha utiwe saini na rais wa Marekani ili kuwa sheria. Kulingana na Wall Street Journal, huu ndio msaada mkubwa zaidi wa kijeshi kuwahi kutolewa na Marekani kwa Israeli tangu kuanza mashambulizi ya utawala huo haramu dhidi ya watu wa Ukanda wa gaza huko Palestina mnamo Oktoba 7 mwaka jana. Tangu baada ya Vita vya Pili vya Dunia, Israel imenufaika zaidi na msaada wa kijeshi wa Marekani kuliko nchi nyingine yoyote, na imekuwa ikiungwa mkono na vyama vya Republican na Democratic kwa muda mrefu. Tangu baada ya kuanza mashambulio ya jes

Kamanda Mwandamizi: Israel imeshindwa na Muqawama Ghaza, viongozi watamatishe vita

Image
  Yitzhak Barik, Jenerali mstaafu wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel amekiri kuwa jeshi la utawala huo haramu limeshindwa na Muqawama wa Palestina katika vita vya Ukanda wa Ghaza na kutaka viongozi wa utawala huo watangaze utamatishaji wa vita hivyo. Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la habari la Palestina SAMA, Jenerali Barik amebainisha kuwa, malengo ya utawala haramu wa Israel yaliyopelekea kuanzisha mashambulio dhidi ya Ghaza bado hayajafikiwa na akasema, Israel inapaswa kutangaza uhitimishaji wa vita huko Ghaza.   Barik ameongeza kuwa, kuivamia kijeshi Rafah, mji wa kusini mwa Ukanda wa Ghaza, hakutausaidia vyovyote utawala huo, kwa sababu Israel imeshindwa katika vita na Muqawama.   Jenerali huyo mstaafu wa jeshi la utawala wa Israel unaofanya mauaji ya kimbari ametamka bayana kuwa, hakuna nguvu inayoweza kuuangamiza moja kwa moja Muqawama ili usiwepo tena. Wanamuqa

Hizbullah yatungua ndege ya kivita isiyo na rubani ya Israel ya Hermes 450 kusini mwa Lebanon

Image
  Harakati ya Mapamabano ya Kiislamu (Muqawama) ya Hizbullah ya Lebanon imesema wapiganaji wake wameiangusha ndege ya kisasa isiyo na rubani ya kivita na kijasusi ya utawala haramu wa Israel kusini mwa Lebanon baada ya kukiuka anga ya nchi hiyo. Katika taarifa Jumapili, Hizbullah imesema imetungua ndege hiyo ya kivita ya Israel aina ya Hermes 450 katika eneo la al-Aishiya kusini mwa Lebanon. Hizbullah imeongeza katika taarifa yake kwamba ndege hiyo isiyo na rubani ya Israel iliangushwa wakati "ilipokuwa ikiwashambulia wananchi waheshimiwa na wenye kusimama kidete." Saa chache baadaye, jeshi la utawala haramu wa Israel lilikiri katika taarifa yake kwamba moja ya ndege zake zisizo na rubani ilitunguliwa kwa kombora la nchi kavu hadi angani wakati ikiwa katika operesheni kwenye anga ya Lebanon. Ndege isiyo na rubani ya Hermes 450, ambayo imetengenezwa na kampuni ya Elbit ya Israel, hutumika kwa ajili ya ujasusi na inaweza pia kubeba hadi makombora ma

HAMAS: Msaada mpya wa Marekani kwa Israel ni kwa ajili ya kuendeleza mauaji ya umati

Image
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imeilaani Marekani kwa kupasisha msaada mwingine kwa utawala wa Kizayuni na kusema kuwa msaada huo ni kwa ajili ya kuendeleza mauaji ya kimbari yanayofanywa na Israel dhidi ya Wapalestina. Shirika la habari la IRNA limenukuu taarifa ya HAMAS iliyotolewa jana Jumapili ikilaani vikali msaada mpya wa Washington kwa utawala wa Kizayuni na kusisitiza kuwa, hatua ya Bunge la Marekani ya kupasisha msaada huo inazidi kuonesha jinsi dola hilo la kibeberu linavyoshiriki moja kwa moja kwenye mauaji ya umati yanayofanywa na utawala wa kifashisti wa Israel dhidi ya Wapalestina wasio na hatia. Harakati ya HAMAS imeongeza kuwa, serikali ya Joe Biden huko Marekani inahusika moja kwa moja kisiasa, kisheria na kimaadili katika jinai za kivita za utawala wa Kizayuni. Wanawake na watoto wadogo wa Palestina, wahanga wakuu wa jinai za Marekani na Israel  

Mufti Mkuu wa Russia: Kiongozi Muadhamu wa Iran anastahiki kupongezwa

Image
Mkuu wa Idara ya Masuala ya Kidini ya Waislamu ya Russia amesema kuwa, mwito unaotolewa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei wa kuwataka watu wote duniani kuthamini masuala ya kidini na kimaadili unastahiki kupongezwa. Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, Mufti Mkuu wa Russia, Sheikh Rawil Ğaynetdin (راویل عین‌الدین) ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Masuala ya Waislamu nchini humo amesema kuwa, juhudi zote za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya nchini Iran zimeelekezwa kwenye kuleta umoja na mshikamano katika umma wa Kiislamu na kwa wanadamu wengine duniani na huko ni katika kutekeleza kivitendo amri za Mwenyezi Mungu.  Sheikh Ğaynetdin (عین‌الدین) pia amesema, msimamo wake huo unawakilisha Waislamu milioni 25 wa Russia na Baraza la Ulama la nchi hiyo kumpongeza Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya nchini Iran akimmkhutubu kwa kumwa

Wapiganaji wa Kiislamu Iraq walenga kambi ya jeshi la Israel kuunga mkono Wapalestina

Image
  Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Iraq imetangaza kulenga ngome "muhimu" ya utawala haramu wa Israel katika Milima ya Golan ya Syria inayokaliwa kwa mabavu na utawala huo ghasibu. Harakati hiyo inayoyaleta pamoja makundi yote ya Kiislamu yanayopambana na ugaidi Iraq imetoa taarifa ikisema imelenga ngome hiyo ya Israel kwa kutumia ndege za kivita zisizo na rubani. Harakati hiyo imesemaa operesheni hiyo  ni "katika kuendeleza vita dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel na kuunga mkono watu wetu huko Gaza wanaokabiliwa na mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na Israel. Hivi karibuni pia Harakati ya Kiislamu ya Iraq ilitangaza kuwa imeshambulia maeneo muhimu katika mji wa Eilat, ulioko kusini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Aidha wapiganaji hao wa Muqawama wa Kiislamu wa Iraq wamelenga Kambi ya Anga ya 'Ovda' ya Wazayuni katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu kwa kut