FAB-3000: Urusi imeanza kutumia tena mabomu hatari
Moja ya sababu za kuanguka mikononi mwa Urusi mji wa Avdeevka ni mashambulio makubwa ya angani. Makombora ya FAB-500 yana uzito wa nusu tani.
Wanaharibu majengo na barabara. Vifaa vya Kikosi cha Wanajeshi wa Ukraine, vilivyoko kilomita moja kabla ya mstari wa mbele viliharibiwa vibaya.
Jeshi la Anga la Kikosi cha Wanajeshi wa Ukraine katika miezi ya hivi karibuni lilitangaza kuangusha ndege 13 za kivita za Urusi.
Hivi karibuni, chaneli ya Urusi ya Wizara ya Ulinzi, iliripoti kwamba Waziri wa Ulinzi Sergei Shoigu alitembelea moja ya kiwanda kikubwa cha kijeshi.
Ripoti hiyo ilizungumza juu ya kuongezeka mara mbili utengenezaji wa makombora ya FAB-1500, lakini zaidi ya yote ilieleza juu ya habari kuhusu kuanza tena kwa mradi wa FAB-3000.
Mabomu haya kutoka angani yana kilo 1,400 za vilipuzi - yana uwezo mkubwa wa kufanya uharibifu.
Jeshi la Soviet lilitumia mabomu kama hayo wakati wa uvamizi wa Afghanistan katika miaka ya 1980. Kwa makombora hayo, waliizingira Kabul.
Mara ya mwisho Warusi walitumia FAB-3000 ilikuwa wakati wa kuzingirwa kwa Mariupol. Walitupa mabomu katika eneo la Azovstal, wakitumia fursa ya kutawala kwao angani.
Warusi sio wasiri sana kuhusu malengo yao. Wakati fursa inatokea ya kutenga maeneo ya mijini, huanza kuweka kizuizi baada ya kizuizi.
Shirikisho la Urusi pia hutumia mara kwa mara mabomu ya kuongozwa kaskazini-mashariki mwa Ukraine - katika ukanda wa mpaka kutoka Chernigov hadi mikoa ya Kharkov.
Maisha katika yamekuwa kuzimu. Jinsi wakazi wanavyoondoka katika eneo la Sumy, ambalo liko chini ya mashambulizi ya Urusi.
Takwimu zinasemaje?
Huwekewa mabawa na linatumia satelaiti, FAB-3000 ni silaha yenye nguvu, kanali mstaafu wa Urusi na mchambuzi wa kijeshi aliambia vyombo vya habari vya serikali, Viktor Litovkin alisema ''haya ni mabomu yenye nguvu sana kwa sababu yanasababisha uharibifu mkubwa."
"Mabomu haya yanaharibu kabisa msimamo wowote," aliandika Egor Sugar, askari wa Kikosi cha 3 cha Mashambulizi cha Ukraine.
Wacha turudi kwenye takwimu za jumla. Tangu mwanzoni mwa 2024, ndege za Urusi zimedondosha zaidi ya mabomu 3,500 ya angani katika maeneo Ukraine. Hii ni mara 16 zaidi ya mwaka 2023.
Zaidi ya miezi mitatu ya sasa - wastani wa mabomu 40 kwa siku. Kulikuwa na siku za utulivu, na pia kulikuwa na wakati walilitupa mabomu 150 katika eneo moja, kwa mfano, Avdievka.
Huko Afghanistan, Mujahidina waliunda mtandao wa ambao ukiona ndege zinazoelekea kuangusha FAB – unatoa ishara ya moshi. Hii ilimaanisha kuwa popote ulipo, ilibidi ubadilishe eneo lake mara moja.
Inafaa kukumbuka kuwa jeshi la wanahewa la Urusi mara kwa mara huzindua mashambulizi ya mabomu kulenga miji ya Ukrainia, lakini kamwe huwa hawarushi ndege zenye wa thamani ndani ya Ukraine ipasavyo. Badala yake, wanarusha makombora kutoka mamia ya maili.
Kwa kweli, mabomu ya FAB-3000 yatasababisha hasara kwa Wanajeshi wa Ukraine. Lakini usambazwaji wa ndege za F-16 na idadi ya kutosha ya mabomu ya JDAM, hali ya Kyiv itabadilika. Moscow haitaweza kutumia mabomu makubwa.