Wapiganaji wa Muqawama Iraq washambulia kituo 'muhimu' cha kijeshi cha Israel

 


Kundi la Wapiganaji wa Mapambano ya Kiislamu (Muqawama) Iraq limetangaza kushambulia kituo "muhimu" cha kijeshi cha utawala wa Israel kilichoko kaskazini mwa maeneo yanayokaliwa kwa mabavu katika kuendelea kuwaunga mkono Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, ambao wanastahimili vita vya mauaji ya halaiki ya Israel.

Kundi hilo la Iraq ambalo ni mwavuli wa makundi ya kupambana na ugaidi nchini humo limetoa tangazo hilo katika taarifa mapema leo Jumapili.

Taarifa hiyo inasema ndege kadhaa zisizo na rubani zimelenga eneo la Eilabun ambapo kituo cha jeshi la Israel hapo kimepata hasara kubwa.

Kundi la Wapiganaji wa Mapambano ya Kiislamu (Muqawama) Iraq lilihitimisha taarifa hiyo kwa kusema kwamba operesheni hiyo imefanywa "kwa mshikamano na watu wa Gaza."

Kundi hilo limekuwa likifanya mashambulizi mengi ya aina hiyo tangu tarehe 7 Oktoba, wakati utawala haramu wa Isarel ulipoanzisha vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.

Hivi majuzi, Kundi la Wapiganaji wa Mapambano ya Kiislamu Iraq lilisema lililenga vituo vya anga vya jeshi la Israel vya  Ovda na Speer katika maeneo ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu, kwa kutumia ndege zisizo na rubani.

Jumapili iliyopita, muungano huo ulitangaza kufanya mashambulizi mengine ya ndege zisizo na rubani dhidi ya "jengo la makao makuu" la wizara ya vita ya Israel katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China