Mkuu wa Ujasusi wa jeshi la Isrel ajiuzulu

 


 

Mkuu wa kijasusi wa jeshi la Israel amejiuzulu, akisema alichukua jukumu la kushindwa kabla ya shambulio la Hamas dhidi ya Israel tarehe 7 Oktoba.

Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) lilisema Meja Jenerali Aharon Haliva atastaafu pindi mrithi wake atakapochaguliwa.

Katika barua, alikiri kwamba kurugenzi yake ya ujasusi "haikutimiza kazi tuliyokabidhiwa".

Yeye ndiye mtu wa kwanza mkuu kujiuzulu kutokana na shambulio hilo ambalo lilikuwa baya zaidi katika historia ya Israel.

Wanajeshi na maafisa wa ujasusi wa Israel walikosa au kupuuza maonyo mengi kabla ya mamia ya watu wenye silaha wa Hamas kuvunja uzio wa mpaka wa Gaza siku hiyo na kushambulia jamii za karibu za Israel, kambi za kijeshi na tamasha la muziki.

Takriban Waisrael 1,200 na raia wa kigeni - waliuawa na wengine 253 walirejeshwa Gaza kama mateka, kulingana na hesabu za Israel.

Israel ilijibu kwa kuanzisha vita vyake vikali zaidi kuwahi kutokea Gaza kwa malengo ya kuangamiza Hamas na kuwakomboa mateka.

Zaidi ya Wapalestina 34,000 huko Gaza - wengi wao wakiwa watoto na wanawake - wameuawa katika mzozo huo, wizara ya afya ya eneo hilo inayoendeshwa na Hamas inasema.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China