Urusi yapinga msaada mpya wa Marekani kwa Ukraine
- Get link
- X
- Other Apps
Sheria iliopo tangu Urusi ilipovamia Ukraine kwa kiwango kikubwa ni kwamba kile ambacho ni kizuri kwa Kyiv ni kibaya kwa Moscow.
Jumamosi iliyopita ilileta habari njema kwa serikali ya Ukraine.
Bunge la Wawakilishi la Marekani lilipiga kura kuunga mkono kifurushi cha msaada cha $61bn (£49bn) kwa Kyiv, ambacho kitatumika kulipatia jeshi lake silaha.
Bunge pia liliidhinisha muswada ambao utaruhusu kukamatwa na kuhamishiwa Ukraine mali ya Urusi iliyohifadhiwa Marekani.
Miswada hiyo sasa inapelekwa kwa Seneti ili kuidhinishwa.
Haishangazi, ni kwanini hatua hii haikupokelewa vyema mjini Moscow.Rais wa zamani Dmitry Medvedev alilaani "dola bilioni 61 za umwagaji damu".
Alitoa wito wa kuwepo kwa Vita vipya vya Wenyewe kwa Wenyewe kwa Waamerika ambavyo "hatimaye vitasababisha kuvunjika vibaya kwa himaya ya uovu ya Karne ya 21, Marekani".
Katika kipindi chake kikuu cha televisheni cha serikali Jumapili usiku, mtangazaji Vladimir Solovyov alielezea wazo la kuhamisha mali ya Urusi hadi Ukraine kama "kitendo cha ugaidi wa kifedha".
"Ikiwa watapitia hili," Bw Solovyov alisema, "basi katika ngazi ya Jimbo la Duma na serikali, lazima tuitangaze Marekani kuwa gaidi wa kifedha."
Aliongeza kuwa sasa anaamini vita kati ya Urusi na Nato "haviwezi kuepukika".
- Get link
- X
- Other Apps