Biden apata shinikizo la kuruhusu silaha za Marekani kuishambulia Urusi

 .

Shinikizo linaongezeka kwa Rais wa Marekani Joe Biden kuruhusu Ukraine kutumia silaha zinazotolewa na nchi za Magharibi kushambulia eneo la Urusi.

Washirika kadhaa wa Marekani wiki hii waliashiria kuwa wako tayari kwa uwezekano huu.

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameonya kuhusu "athari kubwa", hasa kwa kile alichokiita "nchi ndogo" barani Ulaya.

Siku ya Jumatano, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alisema msimamo wa Washington kuhusu suala hilo "utabadilika na kurekebishwa" kulingana na mabadiliko ya hali ilivyo vitani. Kwa sasa yuko katika mji mkuu wa Czech, Prague, kwa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Nato.

Msemaji wa usalama wa taifa wa White House John Kirby alisema jioni Jumatano kwamba ingawa uungaji mkono wa Marekani kwa Ukraine umebadilika, "hivi sasa, pia hakuna mabadiliko katika sera yetu".

Ukraine imekuwa ikijitahidi kukabiliana na mashambulizi ya Urusi mashariki mwa nchi hiyo, huku jiji la Kharkiv likikumbwa na mashambulizi mabaya ya wiki kadhaa, ambayo mara nyingi huanzishwa na Urusi kutoka kwa vituo vya kijeshi karibu na mpaka wa Ukraine.

Kauli ya Bw Blinken, wakati wa safari yake barani Ulaya, ilifuatia maoni ya moja kwa moja zaidi yaliyotolewa mapema wiki hii na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ambaye alisema Ukraine inapaswa "kuruhusiwa" kutumia silaha zinazotolewa na nchi za Magharibi dhidi ya maeneo ya kijeshi katika ardhi ya Urusi - ingawa hailengi raia kabisa.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo