Dakika 34 zilizopitaMaandamano nchini Israel yataka Netanyahu ajiuzulu

 .

Maelfu ya Waisraeli waliandamana siku ya Jumamosi, katika miji mbalimbali, dhidi ya serikali ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, wakitaka makubaliano ya kuwarejesha mateka wa Israel huko Gaza, huku familia za mateka zikimtaka Waziri Mkuu wa Israel ajiuzulu.

Kulingana na gazeti la Kiebrania Haaretz liliripoti, maandamano hayo yalifanyika “siku chache baada ya kutolewa kwa video inayoonyesha sehemu ya kutekwa nyara kwa ambao walichukuliwa mateka siku hiyo.“

Maandamano hayo yalianza Tel Aviv, Haifa, Jerusalem, Beersheba, na karibu na makazi ya kibinafsi ya Netanyahu huko Caesarea. Polisi wa Israel waliwakamata waandamanaji kadhaa, kulingana na picha zilizosambazwa kupitia mashirika ya habari.

Jeshi la Israel limeendelea kushambulia kwa mabomu Ukanda wa Gaza na maeneo ya mji wa Rafah, jana Jumamosi, siku moja baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki kutoa amri inayoitaka Israel kusitisha mashambulizi yake dhidi ya Rafah na kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingia.

Madaktari wa Kipalestina walisema kuwa zaidi ya watu 40 waliuawa katika mashambulio hayo katika maeneo tofauti ya Ukanda huo.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China