Drone tano zilipiga mkoa wa Kharkiv huko Ukraine na kusababisha moto



Jengo la makaazi limeharibiwa baada ya shambulizi la makombora la Russia huko Kharkiv, Ukraine. May 14, 2024.
Jengo la makaazi limeharibiwa baada ya shambulizi la makombora la Russia huko Kharkiv, Ukraine. May 14, 2024.

Rais Zelenskyy  alisafiri Alhamisi kwenda Kharkiv kukutana na maafisa wa kijeshi huku mashambulizi ya Russia yakifanyika katika mkoa huo.

Tahadhari ya muda mrefu ya mashambulizi ya anga kwa sehemu kubwa ya mkoa wa kaskazini mashariki wa Kharkiv nchini Ukraine imeondolewa mapema Ijumaa kufuatia ripoti kuwa mashambulizi ya drone za Russia na onyo la makombora katika mji wa Kharkiv.

Takriban drone tano zilipiga Kharkiv, gavana wa mkoa Oleh Syniehubov amesema. Kharik ni mji wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine. Wilaya ya Osnovyancky mjini humo ilipigwa katika shambulizi hilo na kusababisha moto, Meya Ihor Terekho amesema.

Bado haiijulikani kama kuna mtu yeyote aliyejeruhiwa au kuuawa katika shambulizi. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisafiri Alhamisi kwenda mji wa Kharkiv na kukutana na maafisa wa kijeshi huku mashambulizi ya Russia yakifanyika katika mkoa huo.

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy.
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy.

Zelenskyy alisema kwenye Telegram kwamba hali huko Kharkiv ni ngumu sana lakini kwa ujumla imedhibitiwa. Mwelekeo bado ni mgumu sana, tunaimarisha vitengo vyetu, Zelenskyy alisema kufuatia mkutano katika mji huo na kamanda wake wa juu pamoja na viongozi wa juu wa kijeshi.

Russia imedai udhibiti wa vijiji kadhaa katika mkoa wa Kharkiv katika siku za hivi karibuni, na maendeleo hayo ya Russia yalisababisha Zelenskyy kufuta ziara kadhaa zilizopangwa za nje ya nchi. Wakati wa ziara hiyo huko Kharkiv, Zelenskyy alikutana na wanajeshi waliojeruhiwa ambao walikuwa wakipata huduma katika kituo kimoja cha matibabu.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo