Fahamu mashirika ya ujasusi yenye uwezo mkubwa duniani

 

Wataalamu wa usalama wanapozungumza kuhusu kulinda nchi, kipaumbele chao cha kwanza ni kuwa na wakala imara wa kijasusi. Ndio maana nchi kote ulimwenguni hutumia pesa nyingi zaidi kusasisha na kukuza uwezo wao .

Ujasusi ndio 'kiini tete' cha kila nchi na ujasusi wake wa nje na wa ndani unazingatia masilahi na usalama wa kitaifa.

Shirika la Kitaifa la Ujasusi ndilo ulinzi wa kwanza wa taifa, na ndilo shirika linalohusika na kupata taarifa za siri, na dhana za udukuzi zinazofanywa na nchi, lakini si nchi zote zinazoweza kuwa na nguvu sawa za kiuchumi na kijasusi.

Haya hapa mashirika matano ya kijasusi yenye nguvu na ushawishi mkubwa zaidi ulimwenguni.

1.Shirika la ujasusi la Marekani CIA

CIA ilianzishwa mwaka wa 1947. Ni bora kitaalam kuliko mashirika mengine mengi ya kimataifa na inajua mengi kuhusu matukio ya kimataifa.

CIA ina jukumu la kukusanya taarifa za kigeni, wakati mwingine Marekani. Idadi ya maafisa wa ujasusi katika shirika hilo haijatangazwa rasmi, lakini wanaaminika kuwa miongoni mwa watu wenye nguvu na walioendelea kifedha duniani. CIA inaongozwa na William J. Burns

.

Chanzo cha picha, Getty Images

2. Shirika la kijasusi la Israel Mossad

Mossad ilianzishwa mwaka 1949, mwaka mmoja baada ya kuundwa kwa Israel. Israeli ni taifa la Kiyahudi katikati ya nchi tano za Kiarabu. Kwa kawaida, walihitaji wakala kama Mossad kuweka jicho ili kuwachunguza adui zake.

Ni shirika muhimu sana kwa Israeli na linafanya shughuli nyingi katika sehemu nyingi za ulimwengu.

Utamaduni wa Mossad ni kujiandaa kwa hatari kubwa, ambayo zinatokana na hali ngumu iliyokuwepo wakati wa kuanzishwa kwake.

Katika historia ya Israeli mara kwa mara imejikuta katika vita na ulimwengu wa Kiarabu au katika hali ya migogoro. Leo, Israeli ni nguvu kubwa, lakini utamaduni wa Mossad haujabadilika.

Mi6

Chanzo cha picha, Getty Images

3. Shirika la ujasusi Uingereza MI6

Likiwa na makao yake makuu huko London, lilianzishwa mnamo Julai 4, 1909.

Wakala huu hukusanya taarifa zinazohusiana na usalama wa taifa ndani na nje ya nchi.

MI6 ni mojawapo ya mashirika ya kijasusi yenye nguvu zaidi duniani, na linaongozwa na Richard Moore.

.

Chanzo cha picha, EPA

4: Shirika la ujasusi la Pakistan ISI

ISI ni wakala wa kitaifa wa kijasusi wa Pakistan na ndio kiini cha usalama wa kitaifa wa nchi hiyo.

ISI ina makao yake makuu mjini Islamabad na ilianzishwa mwaka 1948 na kwa sasa inaongozwa na Nadeem Anjum.

Inasemekana kuwa chombo chenye nguvu zaidi nchini Pakistan na ndicho chombo kinachoaminika zaidi nchini humo.

5. Shirika la Ujasusi la Urusi GRU

GRU ni shirika la ujasusi la Urusi lililoanzishwa mnamo 1992.

Ilianzishwa baada ya kuanguka kwa Umoja wa Kisovyeti mwaka 1990 na nafasi yake kuchukuliwa na KGB yenye nguvu.

Taasisi hii iliimarishwa na ujio wa rais Rais Purin.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo