Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo

 .

Msemaji wa Brigedi za Al-Qassam Abu Ubaida, - tawi la kijeshi la Hamas, ametangaza kuwakamata wanajeshi wa Israel katika Ukanda wa Gaza.

Alisema, katika hotuba yake iliyorekodiwa, kwamba wapiganaji wa Al-Qassam walifanikiwa kuwakamata wanajeshi kaskazini mwa Ukanda wa Gaza kwa "kuwarubuni wanajeshi wa Israel kwenye moja ya handaki."

Alisema kwamba hali za wanajeshi waliokuwa kwenye handaki ni kati ya waliofariki, waliotekwa na kujeruhiwa.

Abu Ubaida aliendelea: “Mujahidina wetu waliweza kukamata wanajeshi wa Israeli kutoka katika kikosi kilichoko kambi ya Jabalia.

Ameongeza kuwa vikosi vya Al-Qassam walifanya makumi ya operesheni dhidi ya wanajeshi wa Israel katika kipindi cha zaidi ya wiki mbili huko Rafah na Beit Hanoun - Erez.

Hata hivyo, msemaji wa jeshi la Israel Daniel Hagari alikanusha habari hizo kwenye akaunti yake ya mtandao wa X, akisema: "Ufafanuzi: Hakuna tukio la kuwateka nyara wanajeshi."

Jeshi la Israel limeendelea kushambulia kwa mabomu Ukanda wa Gaza na maeneo ya mji wa Rafah, leo Jumamosi, siku moja baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki kutoa amri inayoitaka Israel kusitisha mashambulizi yake dhidi ya Rafah na kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingia.

Madaktari wa Kipalestina walisema kuwa zaidi ya watu 40 waliuawa katika mashambulizi hayo katika maeneo tofauti ya Ukanda huo.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni