Houthi: Yemen kuongeza vikosi vya kupambana na Israel 'katika ubora na wingi'

 

 Houthi: Yemen kuongeza vikosi vya kupambana na Israel 'katika ubora na wingi'


Kiongozi wa Ansarullah Abdul-Malik al-Houthi anasema vikosi vya Yemen vitaendeleza operesheni zao za kijeshi na kuziongeza "katika ubora na wingi" ili kuunga mkono Wapalestina katika vita vya Israel dhidi ya Gaza.

Vikosi vya Yemen vimekuwa vikilenga meli zinazoelekea katika bandari za Israel na nyingine zenye uhusiano na utawala unaowakalia kwa mabavu katika eneo la Bahari Nyekundu tangu mwezi Novemba. Baadaye walipanua wigo wa shughuli zao hadi Bahari ya Hindi na kusema kwamba wangelenga pia meli zozote zinazoelekea bandari za Israel katika Bahari ya Mediterania.

Katika hotuba ya televisheni siku ya Alhamisi, al-Houthi alisema meli 129 zimelengwa tangu kuanza kwa operesheni "ambayo ni idadi kubwa".

"Hakuna kushuka kwa kiwango cha oparesheni zetu, lakini kupunguzwa kwa usafirishaji wa meli za Amerika na Uingereza kwenda Palestina inayokaliwa," alisema, akipuuza madai kadhaa kwamba Yemen imepunguza mashambulizi yake.

Wiki hii, vikosi vya Yemen vimefanya operesheni 12 katika Bahari Nyekundu, Bahari ya Arabia, Bahari ya Hindi na Bahari ya Mediterania, Houthi alisema.

"Operesheni inaendelea katika mfumo wa awamu ya nne na itaongezeka kwa wingi na ubora."

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo