Ismail Haniyah: Raisi Raisi aliamini Palestina kuwa suala kuu la Kiislamu ulimwenguni

 

  • Ismail Haniyah: Raisi Raisi aliamini Palestina kuwa suala kuu la Kiislamu ulimwenguni

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas , Ismail Haniyah amepongeza misimamo ya marehemu rais wa Iran Shahidi Ebrahim Raisi ya kuunga mkono Palestina.

Ameyasema hayo alipokuwa akiwahutubia mamilioni ya watu waliokusanyika mjini Tehran Jumatano asubuhi katika Swala ya Maiti ya kihistoria ya mazishi ya Rais Raisi, Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir-Abdollahian, na maafisa wengine waliopoteza maisha katika ajali mbaya ya helikopta siku ya Jumapili kaskazini magharibi mwa nchi.

Haniyah amesema katika mkutano wake na Raisi katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, hayati rais wa Iran alisisitiza kuwa Palestina ndilo suala kuu katika ulimwengu wa Kiislamu.

'Raisi aliamini kuwa muqawama ulikuwa chaguo la kimkakati la kuandaa njia ya ukombozi wa Palestina', Haniyah amesema, akimnukuu rais huyo wa zamani akisema kuwa muqawama wa Palestina ndio mstari wa mbele wa mapambano.

Haniyah ameongeza ameongeza kwamba Raisi alisema katika mkutano huo kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kuliunga mkono taifa la Palestina hadi lifikie lengo lake.

Kiongozi Muadhamu akiongoza Swala ya maiti ya mashahidi waliopoteza maisha katika ajali ya karibuni

Mkuu huyo wa Hamas amesema hayati Rais wa Iran pia aliitaja Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa kuwa tetemeko la ardhi ambalo liliutikisa utawala wa Kizayuni na kuanzisha mabadiliko makubwa duniani.

Rais Raisi, Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir-Abdollahian, na ujumbe walioandamana nao walikufa shahidi baada ya helikopta iliyokuwa imewabeba kuanguka katika mkoa wa kaskazini-magharibi wa Azarbaijan Mashariki Mei 19, 2024. Miili yao ilipatikana Jumatatu baada ya operesheni kubwa ya kuwasaka usiku mzima.

Iran iko katika maombolezo ya kitaifa ya siku tano huku misafara ya mazishi ya mashahidi ikiwa inaendelea katika miji mingi. Rais Raisi anatarajiwa kuzikwa kesho Alhamisi kwenye Haram Takatifu ya Imam Ridha (AS) huko Mashhad, kaskazini mashariki mwa Iran.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China