" Israeli, kwa bahati mbaya tuko kwenye harakati ya kuwa taifa lililolotengwa" - Alon Pinkas
s
Zaidi ya miezi saba baada ya mashambulizi ya Oktoba 7 ambayo yalizua vita huko Gaza, maoni ya umma ya kimataifa yanaonekana kuwa ya kugeuka.
Mshikamano wa awali ambao Israeli iliupata baada ya shambulio la Hamas umesababisha maandamano makubwa na ukosoaji mkali, hata kutoka kwa nchi washirika wa jadi.
Mateka wengi wa Israel waliotekwa nyara na Hamas hawajulikani waliko, wakati viongozi wa kijeshi wa kundi la Kiislamu la Palestina - kama Yahya Sinwar - wamejificha chini ya ardhi ili kuepuka mashambulio makali ya kijeshi yaliyoamriwa na serikali ya waziri mkuu Israel, Benjamin Netanyahu, katika Ukanda wa Gaza.
Kwa juu juu, hata hivyo, zaidi ya Wapalestina milioni moja wamekimbia makazi yao na zaidi ya 35,000 wamekufa, kwa mujibu wa mamlaka ya afya ya Gaza, kufuatia mashambulizi ya Israel ambayo yamesababisha sehemu kubwa ya Ukanda wa Gaza kuwa magofu.
Hii imesababisha, pamoja na mambo mengine, maandamano katika vyuo vikuu na katika mitaa ya miji kadhaa duniani; kutambuliwa kwa taifa la Palestina na nchi za Ulaya kama Uhispania, Norway na Ireland, na kesi za kisheria mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), ambapo Israel inatuhumiwa kwa mauaji ya kimbari, pamoja na uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.
Kuhusu kuzorota kwa vita huko Gaza, BBC Mundo ilizungumza na Alon Pinkas, ambaye aliwahi kuwa mkuu wa majeshi chini ya mawaziri wanne wa mambo ya nje wa Israel na kushiriki katika mazungumzo kati ya Israel na Palestina yaliyofuatia mkutano wa Camp David wa mwaka 2000.
Pinkas ambaye pia alikuwa balozi na balozi mdogo wa Israel mjini New York, ni miongoni mwa watu wanaokosoa namna vita hivyo vimekuwa vikipiganwa, na katika mahojiano haya anaonya kuwa iwapo Netanyahu atadumisha sera ya sasa, nchi yake itazidi kutengwa vibaya sana.
Israel ilipata uungwaji mkono kutoka sehemu kubwa ya dunia baada ya Hamas kuua watu 1,200 na kuwateka nyara zaidi ya 200 katika shambulio lake la Oktoba 7. Lakini, miezi saba baadaye, msaada huu unaonekana kutoweka. Wengi wanaona Israeli zaidi kuwa mchokozi kuliko mwathiriwa. Nini kimetokea?
Naam, mambo mawili yalitokea ya kwanza inahusu ulipizaji kisasi wa kijeshi unaofanywa na Israel. Ninaweza kuelewa sababu, naweza hata kuhalalisha hisia, lakini usawa umeendelea kwa muda mrefu sana na kabla ya kujua - wiki 3 au 4 baada ya Oktoba 7 - ulimwengu ulionyeshwa matukio ya uharibifu, mauaji na vifo vya raia, mashambulizi ya kiholela dhidi ya Gaza, na kufuatiwa na uvamizi mkubwa wa Israel wa ardhini kaskazini mwa Gaza.
Na ghafla watu walianza kusahau kilichosababisha haya na kile Hamas ilichokifanya tarehe Oktoba 7, na walichokiona kila siku ni uharibifu wa Israeli wa Gaza. Hili ndilo ilibadilisha maoni ya umma.
Jambo la pili lililotokea ni kwamba baada ya muda, watu walikumbuka hali iliyokuwapo hata kabla ya tarehe 7 Oktoba - kile ambacho watu wanaona kuwa ni uvamizi wa Israel wa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kuizingira Gaza - na watu, haswa waliohusika zaidi kisiasa, waliona kama uthibitisho huo ni wa uhalali zaidi kwamba Israel ni dola ya kikoloni ambayo inapuuza kabisa maisha na matumaini ya Wapalestina.
Serikali ya Israel haikubaliani na wazo kwamba inaendesha vita hivi bila uwiano. Je, unaichukulia vita hii kama vita isiyo na uwiano?
Naam, nadhani ingefaa kushughulikiwa kwa akili zaidi, na hicho ndicho kiini cha ukosoaji wa Marekani kwa Israeli: ikiwa vita vyenyewe ni vita vya haki na matumizi ya njia za kijeshi yanafaa, upeo, ukubwa na muda umekuwa mwingi.
Iwapo Israel ingefaulu, baada ya miezi miwili, labda mitatu, kuiangamiza kabisa Hamas huku ikijaribu kupunguza vita angalau ipigane kwa umakini na kwa dhati kujaribu kupunguza - vifo vya raia, basi nadhani ulimwengu ungeelewa na kuvumilia yaliyotokea.
Ukweli ni kwamba imepita karibu miezi minane na hakuna mwisho unaoonekana mbele.
Afrika Kusini imefungua kesi dhidi ya Israel katika mahakama ya ICJ, Uturuki nayo imesitisha biashara kati ya nchi hizo mbili, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lameshinikiza kutambuliwa kwa taifa la Palestina, maandamano yanafanyika katika miji na vyuo vikuu vingi dhidi ya Israel na hata serikali ya Marekani imesimamisha kwa muda utoaji wake wa msaada wa silaha fulani. Na sasa mwendesha mashtaka wa ICC ameomba hati ya kukamatwa kwa Netanyahu na Waziri wake wa Ulinzi, Yoav Gallant.
Je, Israeli iko katika hatari ya kuwa taifa la lililotengwa?
Inategemea na Israel, inategemea kama kuna mabadiliko ya sera. Maadamu serikali hii iko madarakani na Netanyahu ni waziri mkuu, sioni jinsi siasa itabadilika.
Sidhani Afrika Kusini itafaulu katika ICJ kwa sababu wanabishana kwamba haya ni mauaji ya kimbari na kwamba lazima uthibitishe kuwa kulikuwa na nia ya kufanya mauaji ya kimbari, itakuwa ngumu sana.
Hata hivyo, tukichukua maswali yote uliyoibua na kuunganisha dots zote, tunapata taswira mbaya ya nchi ambayo bado si ya ukabila, lakini inazidi kutengwa na kuelekezwa.
Hivi majuzi ulisema kuwa Israeli ilikuwa taratibu kuelekea kuwa taifa lililotengwa…
Ni sahihi. Ikiwa sera zitaendelea, ikiwa mwelekeo huu wa kisiasa utaendelea, kwa bahati mbaya hii ndiyo njia tunayoelekea.
Ukweli kwamba Israeli haijafanya na, kwa kweli, ilikataa kuwasilisha sera ya baada ya vita jvyake kuihusu Gaza; ukweli kwamba Israeli ilisema haitakaa Gaza, lakini ukweli kwamba imekaa Gaza; ukweli kwamba Israel haifuati ushauri wa Marekani.
Unaongeza vitu hivi vyote pamoja na unaona mchakato wa kile unachokiita - kuwa mtu aliyetengwa taratibu.
Naam, hiyo ilikuwa moja ya nukuu zake. Netanyahu alisema Israel itaendeleza vita hata kama italazimika kufanya hivyo peke yake...
Ni ujinga. Huwezi kufanya hivyo peke yako. Yeye ndiye mwenye kiburi, lakini wakati huo huo hawezi.
Anajua hili haliwezi kufanywa na anasema kuhusu matumizi ya ndani ya Israeli.
Sababu pekee anazosema ni sababu za kisiasa.
Je, unahofia kutakuwa na madhara ya muda mrefu ya sura ya Israeli duniani?
Ndiyo mengi. Nadhani Wamarekani, Wazir iwa mambo ya nje Antony Blinken, alionya Israeli kwamba ilikuwa ikifanya uharibifu wa kizazi kwa sifa kwa jina lake.
Umetaja mustakabali wa Gaza. Nini maoni yako kuhusu mgawanyiko unaoonekana ndani ya baraza la mawaziri la vita la Israel kuhusu mustakabali wa Gaza? Mjumbe wa baraza la mawaziri Benny Gantz aliweka makataa ya Netanyahu kuwasilisha mpango...
Naam, hapana. Alichouliza ni kwamba Netanyahu awasilishe mpango. Kwa hiyo ni jambo la kufikirika kwamba Netanyahu anaweza kupendekeza mpango ambao hataki kuutekeleza na ambao ungemridhisha Gantz.
Sioni mgawanyiko wowote wa kweli ndani ya baraza la mawaziri la vita kwa sasa.
Lakini Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant alisema kukosekana kwa mpango huo kunaidhuru Israel na anapinga utawala wa kijeshi wa muda mrefu wa Israel juu ya Gaza...
Hilo ni kweli, lakini ni ya kipindi cha baada ya vita na vita bado haijaisha, kwa hivyo siwezi kukuambia kuwa inaakisi aina yoyote ya mgawanyiko ambao ungeleta shida za kisiasa.
Angeweza kufanya hivyo kama Gantz na Gallant wangefanya kazi pamoja na kumpa Netanyahu uamuzi mzito. Sio hotuba ya umma, lakini kauli ya mwisho: wacha tuone mpango vinginevyo tutakudanganya.
Kwa hivyo hii inaweza kuwa muhimu na jambo kubwa, wakati huo huo ni kauli ya kisiasa tu.
Baadhi ya watu wanataja ugumu wa kupata msaada wa kibinadamu kwa Gaza kama ishara ya ukosefu wa huruma wa Israeli kwa raia wa Gaza. Utawaambia nini?
Kulikuwa na ukosefu wa huruma kwa uharibifu na maumivu ambayo Israeli iliyapata mnamo Oktoba 7.
Ni baada ya shinikizo kali la Marekani ndipo Israel iliporuhusu msaada huu wa kibinadamu kufika, na nadhani unajua kuwa Israel haiwezi kumudu kuendelea kuonekana kama nchi inayozuia misaada ya kibinadamu.
Ukweli kwamba Netanyahu haonekani kukubali Mamlaka ya Palestina inayoongoza Gaza, operesheni ya sasa ya Rafah na ukweli kwamba serikali yake haionekani kuwa na uwezo au utayari wa kumaliza mashambulio dhidi ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ni mambo yanayotumiwa na wakosoaji wa 'Israeli. Wanasema kwamba Israeli wanataka kuteka maeneo yote “kutoka mto mpaka baharini”…
Ni ujinga. Maoni ya umma yanapinga, hayawezi kuwa ukweli kivitendo na unachosikia kutoka kwa wanasiasa wa mrengo wa kulia ni upuuzi tu.
Haitatokea. Ninaelewa wakosoaji wanaotumia hili kama suala la kuipinga Israeli, lakini hilo halitafanyika.
Wataalamu wengi na watu wanaojiona kuwa marafiki wa Israel nchini Marekani na kwingineko mapema waliitaka Israel kuepuka aina hii ya vita. Walidai kwamba hii ingeinufaisha Hamas. Je, kweli hapakuwa na njia mbadala ya jinsi Israeli walivyopigana vita hivi?
Bila shaka, kulikuwa na njia nyingi mbadala.
Kwa mfano angetishia kufanya uvamizi, fna kuharakisha kwanza apate makubaliano ya kuwaachilia mateka. Kulikuwa na njia zingine kadhaa za kufanya hivi.
Kulikuwa na njia nyingi za kijeshi za kupigana vita hivi tofauti.
Baadhi ya wachambuzi wa mambo wanasema vita hivi vimeitenga zaidi Israel na Wapalestina na kwamba itachukua vizazi kuponya majeraha, lakini wakati huo huo kuna shinikizo kubwa kutoka kwa Marekani na wengine kutaka suluhu ya mataifa mawili.
Je yote haya yataleta suluhisho la serikali mbili kuwa gumu au rahisi?
Hilo ni swali kubwa, lakini hii Inategemea jinsi vita inavyoisha.
Kwa mtazamo wa kwanza, tuko mbali zaidi, lakini pia tunatambua kwamba hali iliyopo haiwezi kudumishwa. Kwa hivyo tuko karibu zaidi, lakini sio kwa serikali hizi.