Je nyota wa ponografia katikati ya kesi iliyomtia hatiani Donald Trump ni nani?

 g

Stormy Daniels ndilo jina la mwanamke aliyetawala katika kesi ya jinai ambayo Rais wa zamani Donald Trump alipatikana na hatia Alhamisi hii katika kesi ya kihistoria iliyofanyika Manhattan.

Jina halisi ni Stephanie Gregory Clifford, ni mwigizaji wa zamani, mwandishi wa maandishi ya skrini na mkurugenzi wa filamu za ponografia , na anadai kuwa mwaka 2006 alikutana na Trump, wakati tayari alikuwa ameoana na mke wake wa sasa, Melania, kitu ambacho mara kwa mara alikanusha.

Majaji wa mahakama ya New York wanaonekana kumuamini, kumpata rais huyo wa zamani na hatia ya mashtaka 34 yanayohusiana na kughushi rekodi za uhasibu ili kuficha malipo ambayo wakili wa Trump angemlipa Clifford kununua ukimya wake kuhusu uhusiano huo na hivyo kumlinda katika kampeni za uchaguzi 2016 .

Sasa hakimu katika kesi hiyo anatakiwa kutoa hukumu hiyo, jambo ambalo litafanyika Julai 11.

"Mimi ni mtu asiye na hatia sana ," Trump alisema wakati akitoka nje ya mahakama, wakati wa kesi ya uchaguzi wa rais mnamo Novemba 5.

Waanzilishi wa tasmia

f

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Stormy Daniels alikuwa na kazi nzuri kama mwigizaji wa ponografia na mkurugenzi katika miaka ya 2000.

Stephanie Gregory Clifford alizaliwa Baton Rouge, katika jimbo la kusini la Louisiana, mwaka wa 1979, na ni mpenzi wa kuendesha farasi.

Akiwa mtoto, ndoto yake ilikuwa kuwa daktari wa mifugo, lakini baada ya talaka ya wazazi wake, alipokuwa na umri wa miaka 4, alilelewa na mama yake, ambaye alikuwa na wakati mgumu wa kusaidia familia kifedha.

Katika umri wa miaka 17 alianza kufanya kazi kama mcheza dansi ya utupu katika kilabu.

Alipoanza kujulikana zaidi, aliamua kuchukua jina la jukwaa. Akiwa shabiki wa bendi ya rock ya Motley Crue, aliamua kutoa pongezi kwa binti wa mpiga gitaa ya bezi wa kundi hilo, ambaye jina lake ni Storm. Jina la ukoo ni kwa heshima ya chapa ya whisky ya Jack Daniel.

Mnamo 2000 alianza kazi yake kama muigizaji wa filamu za watu wazima na kampuni ya utengenezaji wa Wicked Pictures, ambayo alikuwa na kazi nzuri. Pia alishiriki katika filamu za Sin City Studios.

Mnamo 2004 alianza kazi ya kuwa mwelekezi wa filamu za ponografia katika kampuni ya Wicked Pictures na baadaye pia alifanya kazi kama mwandishi wa maelezo ya filamu kwenye skrini.

Mtaalamu wa filamu za watu wazima Kelly Roberts aliiambia BBC kwamba Stormy Daniels alikuwa mwanzilishi katika tasnia hiyo.

"Wakati huo hapakuwa na wakurugenzi wanawake. Haikujulikana. Wote walikuwa wanaume ," alisema.

Kwa kazi yake kama mkurugenzi, Daniels alishinda tuzo kadhaa kutoka kwa jarida la Habari za Video za Watu Wazima (AVN), ikizingatiwa kuwa tasnia ya ponografia ni sawa na Oscars.

Na mnamo mwaka 2014 jina lake liliongezwa kwenye kumbi za umaarufu za jarida la AVN na Shirika la Wakosoaji wa X.

Kulingana na mtengenezaji wa filamu Judd Apatow, ambaye alitoa majukumu yake katika filamu zake mbili, Daniels "si mtu wa kudharau."

"Yeye ni mwanamke mfanyabiashara makini sana na mtayarishaji filamu ambaye amechukua hatamu za kazi yake," Apatow aliambia The New York Times miaka michache iliyopita.

Maelezo ya "Gory" katika kesi

g

Chanzo cha picha, Reuters

Jina lake lilianza kujulikana miongoni mwa umma wakati mwaka wa 2018 alipofanya mahojiano na kipindi cha televisheni cha CBS cha 60 Minutes, ambapo alitoa maelezo ya madai yake ya ngono na Trump.

Haya ni maelezo yale yale ambayo aliyarudia Mei 7 alipochukua msimamo kwa mara ya kwanza wa kutoa ushahidi katika kile kilichokuwa kikitarajiwa sana katika kesi ya Trump.

Mbele ya jopo la mahakama, rais wa zamani na waendesha mashtaka, muigizaji huyo alisema alikutana na Trump katika hoteli katika Ziwa Tahoe mwaka 2006 .

Alisema Trump alikuwa amevalia pajama za hariri na alimuuliza maswali kadhaa ya "biashara" kuhusu familia yake, elimu yake na kazi yake katika tasnia ya filamu ya watu wazima.

Wakati fulani, mfanyabiashara huyo alimweleza kuwa alimpata sawa na bintiye Ivanka, Daniels alishuhudia, akimwambia kwamba watu waliwadharau wote kwa sababu walikuwa wazuri.

"Bi. Daniels, tafadhali eleza kwa kifupi majibu yako," Jaji Juan Merchan alimwambia shahidi.

Katika ushuhuda wake, muigizaji huyo wa zamani wa filamu za ngono alitoa maelezo ya kutisha kiasi kwamba mawakili wa rais huyo wa zamani waliomba kesi hiyo ibatilishwe.

Haya ni pamoja na madai kwamba hawakutumia kondomu au kwamba alimpiga na gazeti , pamoja na majibu anayodaiwa kupata kutoka kwa rais huyo wa zamani kuhusu mke wake.

Jaji Juan Merchan alikiri kwamba kulikuwa na "baadhi ya mambo ambayo yangeachwa bila kusemwa" na kuwataka waendesha mashtaka kutouliza maelezo mahususi kuhusu hali ya kibinafsi ya mkutano wake na Trump.

Kulingana na Daniels, mnamo 2016, baada ya Trump kuzindua kampeni yake ya urais, aligundua kuwa mfanyabiashara huyo na wakili wake Michael Cohen walitaka kununua ukimya wake ili aache kutoa taarifa kumhusu Trump.

Makubaliano hayo yangekuwa ya manufaa kwa kila mtu, Daniels alitangaza, kwa sababu hakutaka mpenzi wake wa wakati huo ajue kuhusu madai ya kukutana kwake na Trump.

Pia alieleza jinsi makubaliano yalivyofikiwa ya kupokea fedha hizo. Alisema alisem alipendekeza kwanza kuuza hadithi yake kumugusu Trump alipojua kwamba kuna mtu mwingine ambaye alikuwa akipanga kufanya hivyo kabla yake.

"Ningependelea kupata pesa kuliko mtu mwingine atengeneze pesa kwa gharama yangu ," alisema.

 

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China