Jeshi la Sudan lakataa wito wa Marekani wa kuzungumza na waasi

  • Jeshi la Sudan lakataa wito wa Marekani wa kuzungumza na waasi

Jeshi la Sudan limekataa wito wa kurejea kwenye mazungumzo ya usitishaji vita na kundii la waasi la RSF kufuatia mazungumzo kati ya kiongozi wa Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken.

Blinken alimpigia simu al-Burhan juzu ambapo alijaribu kumshawishi afanya mazungumzo na waasi wa RSF. Afisa mwandamizi wa Sudan Malik Agar amapinga uingiliaji wa Marekani na kusema: "Hatutakwenda Jeddah (Saudi Arabia) na yeyote anayetutaka atuue katika nchi yetu na kuipeleka miili yetu huko."

Marekani imekuwa ikisiamamia mazungumzo hayo ya waasi na serikali ya Sudan huko Jeddah. Hatahivyo mazungumzo hayo hadi sasa hayajafanikiwa.

Mapigano makali yaliendelea Jumatano katika maeneo ya kaskazini mwa mji mkuu, huku wakaazi wakiripoti mashambulizi makali ya angani na mizinga.

Sudan hataivyo imekaribisha mwaliko wa Misri wa mkutano wa kilele wa makundi ya kisiasa ya kiraia, lakini iliweka masharti kuhusu aina ya makundi na wahusika wa kigeni walioalikwa.

Mapigano ya silaha yalianza huko Sudan Aprili 15 mwaka jana kati ya Jeshi la Sudan (SAF)  linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al Burhan ambaye ni kiongozi wa Sudan na waasi wanaojulikana kama Kikosi cha Usaidizi wa Haraka (RSF) ambao kamanda wao ni Hamdan Dagalo.

Hivi karibuni Justin Brady, Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu (OCHA) nchini Sudan alisema, "leo, Sudan ni mojawapo ya majanga mabaya zaidi ya kibinadamu duniani. Nusu ya wakazi wa Sudan yaani watu milioni 25 wanahitaji msaada wa kibinadamu."

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo