Jeshi la Yemen latekeleza oparesheni tatu za aina yake


  • Jeshi la Yemen latekeleza oparesheni tatu za aina yake

Msemaji wa jeshi la Yemen ametangaza kuwa jeshi hilo limetekeleza oparesheni tatu za aina yake dhidi ya mei tatu katika fremu ya awamu ya nne ya kushtadi mivutano.

Kwa mujibu wa kanali ya Televisheni ya Al-Mayadeen, Brigedia Yahya Saree, Msemaji wa jeshi la Yemen jana Ijumaa aliashiria  operesheni tatu za jeshi la nchi hiyo dhidi ya meli tatu na kusema: Katika operesheni ya kwanza meli ya utawala wa Kizayuni MSC ALEXANDRA ililengwa kwa makombora kadhaa ya balistiki katika Bahari ya Makran. 

Meli ya Israel yalengwa kwa makombora na jeshi la Yemen 

Msemaji wa jeshi la Yemen ameongeza kuwa, katika oparesheni ya pili pia vikosi vya majini vya Yemen, ndege zisizo na rubani na kikosi cha makombora cha nchi hiyo viliipifa meli ya YANNIS yenye mfungamano na kampuni moja ya Ugiriki wakati ilipokuwa ikipita katika Bahari Nyekundu. 

Brigedia Jenerali Yahya Saree amebainisha kuwa, katika oparesheni ya tatu ya jeshi la Yemen, kikosi cha makombora cha jeshi kiliishambulia meli iya ESSEX ya utawala wa kizayuni kwa makombora kadhaa katika bahari ya Mediterania. 

Wakati huo huo, msemaji wa jeshi la Yemen kwa mara nyingine tena alimeonya kampuni zote zinazoshirikiana na utawala wa Kizayuni kwamba meli zao zitalengwa bila ya kujali zinakoelekea katika eneo la oparesheni za jeshi la Yemen.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China