Kamanda wa IRGC: Israel iliweka tayari mamia ya ndege wakati wa operesheni ya Iran

 

  • Kamanda wa IRGC: Israel iliweka tayari mamia ya ndege wakati wa operesheni ya Iran

Kamanda wa ngazi za juu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) amesema utawala wa Kizayuni wa  Israel uliweka mamia ya ndege za kivita katika hali ya tahadhari kwa ajili ya kukabiliana na mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Iran mwezi uliopita.

Brigedia Jenerali Amir Ali Hajizadeh, kamanda wa Kitengo cha Wanaanga cha IRGC alisema Alhamisi kwamba: "Takriban ndege 221 za kivita ziliwekwa katika hali ya tahadhari kuzuia mashambulizi ya Iran."

Ikumbukwe kuwa, Jumatatu, Aprili 1, 2024, utawala wa Kizayuni wa Israel ulishambulia ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus katika shambulio la kigaidi lililopelekea kuuawa shahidi washauri saba wakuu wa kijeshi wa Iran.

Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Iran aliitaja hatua hiyo ya Israel kuwa ni shambulio dhidi ya ardhi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusisitiza kuwa, utawala wa Kizayuni "utaadhibiwa".

Katika kutekeleza ahadi hiyo, Jumapili asubuhi (tarehe 14 Aprili 2024), Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu lilichukua hatua ya kuuadhibu utawala huo wa Kizayuni kwa kuvurumisha ndege zisizo na rubani na makombora kuelekea ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) kupitia operesheni ya kuiadhibu Israel iliyopewa jina la "Ahadi ya Kweli."

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China