Makamba: Mataifa ya Afrika yawe na haki ya kuchagua washirika

 

  • Makamba: Mataifa ya Afrika yawe na haki ya kuchagua washirika

Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania January Makamba Kila taifa la Afrika na bara zima lazima liwe na uwezo wa kujitegemea katika kuchagua washirika wake na kulinda maslahi yake binafsi

Makamba amenukuliwa na Shirika la Habari la Sputnik la Russia akisema: "Sisi [Waafrika] tunaona inakera kushinikizwa kuchagua mshirika huyu mmoja au mwingine."

Aidha amesema uhuru wa kweli na uhuru wa Afrika unaweza kupatikana kwa kujitegemea na kwa umoja.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania pia alikosia mataifa ya kikoloni na mataifa mengine ya Magharibi kwa kujaribu kurejesha satwa yao ya kibeberu  Afrika, jambo ambalo linazifanya nchi kama Niger, Mali, na Burkina Faso "kuwafukuza" wakoloni wao wa zamani.

Makamba ameendelea kusema kuwa: "Nchi za Ulaya, na hasa Marekani, hivi sasa, zinajaribu kurejea tena kwa kasi Afrika."

Hivi karibuni Ufaransa imekuwa ikipata hasara kubwa barani Afrika hasa katika eneo la magharibi mwa bara hilo ambapo viongozi wa Burkina Faso, Mali na Niger walikatisha makubaliano ya kijeshi na wakoloni wao wa zamani.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo