Matokeo uchaguzi Afrika Kusini 2024: ANC yaelekea kupoteza wabunge wengi

Idadi kubwa ya wabunge wa chama tawala cha ANC iko hatarini

Chama tawala nchini Afrika Kusini, African National Congress (ANC), kiko mbioni kupoteza wingi wa wabunge kwa mara ya kwanza tangu kilipoingia madarakani miaka 30 iliyopita, matokeo ya uchaguzi wa bunge wa Alhamisi yanaonesha.

Huku matokeo kutoka zaidi ya 50% ya wilaya za wapiga kura yamehesabiwa hadi sasa, ANC inaongoza kwa 42%, ikifuatiwa na Democratic Alliance (DA) kwa 23%.

Chama cha Umkhonto weSizwe (MK Party) cha Rais wa zamani Jacob Zuma kimepata karibu 11% ya kura na chama cha Economic Freedom Fighters, karibu 10%.

Matokeo ya mwisho yanatarajiwa mwishoni mwa juma.

Wapiga kura wengi wanalaumu ANC kwa viwango vya juu vya ufisadi, uhalifu na ukosefu wa ajira nchini.

Baraza linaloheshimika la Utafiti wa Sayansi na Viwanda (CSIR) na tovuti ya News24 zimekadiria kuwa kura za mwisho za chama hicho zitakuwa karibu 42%, ikiwa ni tofauti kubwa kutoka kwa 57% ilizopata katika uchaguzi wa 2019.

Hili itakilazimu chama kuingia katika muungano na chama kimoja au zaidi ili kuunda wabunge wengi.

Haijulikani ikiwa Rais Cyril Ramaphosa atasalia madarakani, kwani anaweza kukabiliwa na shinikizo kutoka kwa ANC kujiuzulu ikiwa chama kitapata chini ya 45% ya kura za mwisho, alisema Prof William Gumede, mwenyekiti wa shirika lisilo la faida la Democracy Works Foundation. .

EFF na MK pia wana uwezekano wa kumtaka ajiuzulu kabla ya kukubaliana na muungano wowote na ANC.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo