Mtandao mkubwa wa uhalifu kwa njia ya kompyuta wafungwa duniani: Marekani

Mtandao wa kompyuta umefanya matukio ya uhalifu ulimwenguni

Idara za kipolisi kote ulimwenguni kote zimefunga mtandao wa kimataifa wa programu ambao uliiba $5.9bn (£4.65bn) na unahusishwa na uhalifu mwingine, Wizara ya Sheria ya Marekani (DOJ) imesema.

DOJ ilishirikiana na FBI na mashirika mengine ya kimataifa ili kuondoa kile kinachowezekana kuwa mtandao wa kompyuta zilizoathiriwa na programu ambazo ziko chini ya udhibiti wa mtu mmoja.

Raia wa China YunHe Wang, ambaye pia ni mkazi wa St Kitts na Nevis citizen ameshtakiwa kwa kuunda na kuendesha mtandao huo.

Bw Wang anashtakiwa kwa njama ya kufanya ulaghai kwa njia ya mtandao wa kompyuta, njama ya kufanya ulaghai kwa njia ya mtandao na kula njama ya kutakatisha pesa.

Iwapo atapatikana na hatia kwa makosa yote, anakabiliwa na adhabu ya juu zaidi ya miaka 65 jela.

Kulingana na shtaka, kati ya 2014 hadi 2022, Bw.Wang na wengine waliunda na kuendesha mtandao uitwao 911 S5, kutoka kwa seva 150 kote ulimwenguni.

Mtandao huo ulidukuliwa katika zaidi ya anwani milioni 19 za Itifaki ya Mtandao (IP) katika karibu nchi 200, DOJ ilisema.

Anuani ya IP hutambulisha kifaa kwenye mtandao. mtandao huo ulitumika kutekeleza mashambulizi ya mtandaoni, ulaghai mkubwa, unyonyaji kwa watoto, unyanyasaji, vitisho vya mabomu na ukiukaji wa mauzo ya nje, DOJ ilisema.

Marekani ilikadiria kuwa zaidi ya nusu milioni ya madai ya ulaghai ya bima ya ukosefu wa ajira yalitokana na anwani za IP zilizoathirika, na kusababisha hasara ya zaidi ya $5.9bn.

Mtandao huo pia uliwawezesha wahalifu wa mtandao kununua bidhaa kwa kadi za mkopo zilizoibwa au pesa chafu, DOJ ilisema.

Bw Wang inadaiwa aliuza anuani za IP na akapokea takribani $99m, DOJ ilisema.

Inadaiwa alinunua mali Marekani, St Kitts na Nevis, China, Singapore, Thailand na Falme za Kiarabu. Mali yenye thamani ya jumla ya karibu $60m imekamatwa au kutambuliwa ikiwa ni pamoja na Ferrari, Rolls-Royce na saa kadhaa, DOJ ilisema.

Mashirika ya kipolisi nchini Singapore na Thailand, pamoja na kampuni kubwa ya teknolojia ya Microsoft, yalikuwa miongoni mwa mashirika yaliyosaidia katika uchunguzi huo

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo