Mwanafunzi wa miaka 85 asoma shahada yake ya nne

 Lucille Terry hakutaka tu kukaa nyumbani baada ya kustaafu

Mwanafunzi mwenye umri wa miaka 85 ambaye anasoma shahada yake ya nne ya chuo kikuu anasema "hawezi kuketi tu".

Lucille Terry kutoka Cirencester alimaliza shahada yake ya kwanza, katika taaluma ya dawa, katika Chuo Kikuu cha Manchester mnamo 1962.

Atamaliza shahada yake ya nne, ya tatu katika Chuo Kikuu Huria, atakapokuwa na umri wa miaka ya tisini.

Bi Terry alitunukiwa katika sherehe katika kanisa la parokia yake siku ya Jumatatu. Bi Terry, ambaye alifanya kazi ya ualimu, kwa sasa anasomea shahada ya masomo ya kidini, falsafa na maadili.

Mkazi wa Siddington Park pia ana shahada ya masuala ya ubinadamu, saikolojia na ubinadamu na masomo ya kidini, na alifanya masomo ya msingi ya sayansi katika Chuo Kikuu Huria mnamo 1972, kabla ya kusomea cheti chake cha ualimu.

Bi Terry aliamua kwamba hakutaka "kucheza tu mchezo wa mafumbo ya maneno" wakati wa kustaafu kwake. "Siwezi kuketi tu, bila kufanya chochote na kutazama televisheni wakati wote," alisema.

"Binti yangu aliniuliza wiki chache zilizopita, 'Unapenda kufanya nini hasa?'. "Ninapenda kusoma. Ninafurahia."

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo