Mwanaume afariki dunia kwenye injini ya ndege Amsterdam

 .

Mtu mmoja afariki dunia baada ya kuishia kwenye injini ya ndege ya abiria ya KLM katika uwanja wa ndege wa Schiphol mjini Amsterdam.

Kifo hicho kilitokea wakati ndege ya KL1341 ilipokuwa ikijiandaa kuondoka kuelekea Billund, Denmark, Jumatano alasiri.

Shirika hilo la ndege limesema linawahudumia abiria na wafanyakazi walioshuhudia tukio hilo na linaendelea na uchunguzi.

Polisi wa kijeshi wa Netherland pia walisema kuwa wameanza uchunguzi.

Kikosi cha Royal Netherlands Marechaussee kiliongeza katika ujumbe kwenye mtandao wa X kwamba abiria na wafanyikazi wote wameondolewa kwenye ndege.

Marehemu bado hajatambuliwa na ni mapema mno kusema ikiwa ilikuwa ajali au aina ya kujitoa uhai, msemaji aliliambia shirika la habari la Reuters.

Vyombo mbalimbali vya habari vya Uholanzi vimependekeza mwathiriwa anaweza kuwa mfanyakazi anayehusika katika kuelekeza ndege kurudi nyuma kabla ya kupaa.

Picha zilizopatikana na shirika la utangazaji la taifa la Uholanzi NOS zinaonyesha huduma za dharura zinazozunguka ndege ya abiria kwenye uwanja wa ndege - ambapo ndege huegeshwa.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo