Rais Ruto: 'Marafiki wa Kenya' walilipia ndege yangu kwenda Marekani

 Rais wa Kenya William Ruto

Rais wa Kenya William Ruto amesema ndege yake aliyosafiri nayo kwenda Marekani iligharmiwa na walipa kodi wa Kenya kiasi cha chini ya milioni 10

Ruto amesema kuwa baadhi ya marafiki wa Kenya ambão hakuwataja, walitoa ndege hiyo, baada ya kusema kuw angesafiri na ndege ya shirika la Ndege la Kenya.

‘’Nilipoona mjadala Kenya kuhusu ni kwa namna gani nilisafiri kwenda Marekani na gharama mbalimbali zikielezwa kuwa….hii imegharimu milioni 200, hakuna namna ninayoweza kutumia sh milioni 200. Acha niwaambie hapa, hii imeigharimu kiasi cha chini ya shilingi milioni 10’’, alisema Rais Ruto.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo