Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump akutwa na hatia kwa makosa yote katika kesi ya kihistoria

Trump

Donald Trump, rais wa 45 wa Marekani, amekuwa rais wa kwanza wa zamani kupatikana na hatia ya uhalifu.

Trump alipatikana na hatia ya makosa 34 ya kughushi rekodi za biashara ili kuficha malipo ya pesa kwa nyota wa ponografia.

Atahukumiwa Julai 11, siku nne tu kabla ya Chama cha Republican kumchagua rasmi kugombea urais katika mkutano wao wa chama.

Amepinga uamuzi huo na kutangaza kuwa atafanya mkutano na waandishi wa habari Ijumaa asubuhi katika jumba la Trump Tower huko Manhattan.

Athari ya uamuzi huo wa kihistoria bado haijulikani wazi, kwa jinsi inavyoathiri uwezo wa Trump.

Kambi ya Biden ilitoa taarifa, na kuwakumbusha wapiga kura kwamba njia pekee ya kumshinda Trump ni kwenye sanduku la kura, sio chumba cha mahakama.

Mmoja wa mawakili wakuu wa Trump ameiambia Fox News kwamba timu ya wanasheria wa rais wa zamani "inazingatia chaguzi zote" za kukata rufaa.

"Kila kipengele cha kesi hii kiko tayari kwa rufaa," alisema Will Scharf.

"Tutakata rufaa haraka tuwezavyo."

Wakili mwingine muhimu wa timu ya wanasheria wa Trump, Todd Blanche, pia amejitokeza kwenye Fox ambapo alisema kuwa mteja wake hakutendewa haki.

"Tumekuwa tukisema kwa zaidi ya mwaka mmoja kwamba hatukutendewa haki huko Manhattan," alisema.

Baada ya siku mbili za mashauriano, Donald Trump amekutwa na hatia ya mashtaka yote katika kesi yake ya uhujumu uchumi.

Wabunge wa chama cha Democratic na baadhi ya wakosoaji wakubwa wa Donald Trump wamepeleka ujumbe wao kwa X, ambayo zamani ilikuwa Twitter, kujibu hukumu ya hatia ya Trump. Wanakariri madai kwamba "haki imeshinda".

"Leo, majaji kumi wa Marekani walimpata rais wa zamani na hatia ya makosa kadhaa. Licha ya jitihada zake za kuvuruga, kuchelewesha, na kukanusha, haki imetendeka dhidi Donald Trump vivyo hivyo. Na utawala wa sheria ulitawala," Mwakilishi wa California Adam Schiff. aliandika.

Schiff alihudumu katika kamati teule ya Bunge kuchunguza shambulio la tarehe 6 Januari 2021 kwenye Ikulu ya Marekani.

"Majaji wamezungumza. Haki imeshinda," Mwakilishi Jim Clyburn, mwanademokrasia kutoka Carolina Kusini, aliandika kwenye mtandao wa X.

Mwakilishi wa Washington Pramila Jayapal, mwenyekiti wa Baraza la Maendeleo la Congress, aliuita "wakati muhimu kwa uwajibikaji nchini Marekani".

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo