Saa 2 zilizopita15 wafariki dunia kwa joto kali India
Watu kadhaa wamefariki dunia kutokana na magonjwa yanayohusiana na joto kali katika muda wa saa 24 zilizopita huku halijoto ikiendelea kuongezeka kaskazini na katikati mwa India.
Vifo kumi vilirekodiwa katika hospitali ya serikali mkoa wa Rourkela wa Odisha siku ya Alhamisi, wakuu wa hospitali waliambia shirika la habari la Reuters.
Vifo vinavyohusiana na kiharusi cha joto kali pia vimeripotiwa kutoka majimbo ya Bihar, Rajasthan na Jharkhand na mji mkuu wa kitaifa, Delhi.
Joto kali linawadia huku India ikifanya uchaguzi mkuu, ambao matokeo yake yatatangazwa tarehe 4 Juni.