Ubalozi wa Israel nchini Mexico wateketezwa moto katika maandamano ya kupinga mauaji ya Rafah


  • Ubalozi wa Israel nchini Mexico wateketezwa moto katika maandamano ya kupinga mauaji ya Rafah

Waandamanaji waliokuwa na hasira wameuchoma ubalozi wa utawala haramu Israel katika jiji la Mexico City nchini Mexico wakati wakibanisha malamiko yao kuhusu mauaji ya kimbari yanaotekelezwa na Israel huko Gaza.

Waandamanaji wanaounga mkono Wapalestina walishiriki katika "Hatua ya Dharura Kwa Ajili ya Rafah" na walielezea hasira zao mbele ubalozi wa utawala ghasibu Israel. Waandamnaji waliokuwa na hasira walivurumisha mabomu ya kujitengenezea ya Molotov Cocktail katika jengo la ubalozi huo wa Israel.

Aidha waandamanaji waliwarushia mawe polisi wa kutuliza ghasia ili kulipiza kisasi baada ya kurushiwa  mabomu yakuwarushia vitoa machozi.

Mexico, siku ya Jumanne, iliwasilisha tamko la kujiunga na kesi ya Afrika Kusini dhidi ya utawala haramu wa Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) ikiishutumu Israel kwa kutekeleza "mauaji ya kimbari" Gaza.

Maandamano kama hayo yameshuhudiwa kote ulimwenguni kufuatia shambulio la Jumapili jioni la utawala katili wa Israel kwenye kambi ya wakimbizi huko Rafah, na kuua karibu Wapalestina 50.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China