Ujerumani: Emmanuel Macron afungua milango kwa mashambulizi ya Ukraine nchini Urusi

 Emmanuel Macron na Olaf Scholz wanahudhuria mkutano na waandishi wa habari katika nyumba ya wageni ya serikali ya Ujerumani huko Meseberg, kaskazini mwa Berlin, Ujerumani, Jumanne hii, Mei 28, 2024.

 Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alimaliza ziara yake ya kiserikali nchini Ujerumani Jumanne jioni, Mei 28, kwenye Kasri la Meseberg, karibu na Berlin, akiwa na Baraza la Mawaziri la serikali ya faransa na Ujerumani. Kabla ya kuongoza mkutano huu, rais wa Ufaransa na kansela wa Ujerumani, Olaf Scholz, waliandaa mkutano na waandishi wa habari kuelezea vipaumbele vyao.

Olaf Scholz alisema tangu mwanzo wa hotuba yake: vita vya Ukraine ni "wasiwasi wake mkuu" na Emmanuel Macron.

Rais wa Ufaransa ambaye amebaini siku ya Jumanne usiku kwamba Ukraine inapaswa kuwa na uwezekano wa kufanya mashambulizi makubwa katika ardhi ya Urusi. Raia wa Ukraine lazima waruhusiwe "kuangamiza kabisa maeneo ya kijeshi ambayo hutokea mashambulizi yanayowasibu", lakini sio malengo mengine nchini Urusi, amesema rais wa Ufaransa. Katika hali hizi, kulingana na rais Macron, hakuna hatari ya "kuongezeka kwa vita".

Ufaransa bado ina mfumo huo wa utekelezaji nchini Ukraine. Tunaunga mkono Ukraine katika kupinga na kutetea eneo lake, na hatutaki kuongezzeka kwa vita.

Kilichobadilika ni kwamba Urusi imerekebisha mazoea yake kidogo. Ardhi ya Ukraine nashambuliwa kutoka kwa kambi za kijeshi nchini Urusi. Kwa hivyo, tunawaelezeaje Waukraine kwamba tutalazimika kulinda miji hii na, kimsingi, kila kitu tunachokiona kwa sasa karibu na Kharkiv, ikiwa tutawaambia: "hamna haki ya kufikia maeneo ambapo makombora yanarushwa?" Kwa kweli tunawaambia: “Tunawapa silaha, lakini hamuwezi kujilinda.” Kwa hivyo tunabaki katika mfumo huo, tunadhani kwamba lazima tuwaruhusu kugeuza maeneo ya kijeshi ambayo makombora yanarushwa, na kimsingi maeneo ya kijeshi ambayo Ukraine inashambuliwa, lakini hatupaswi kuruhusu kugonga malengo mengine nchini Urusi. na, kwa hakika, uwezo wa kiraia au malengo mengine ya kijeshi.

Kuhusu suala la kutambua taifa la Palestina, kama zilivyofanya Uhispania, Ireland na Norway hivi punde, Emmanuel Macron anaona kuwa haikuwa "mwiko", lakini ametaja kwamba inapaswa kutokea kwa "wakati manufaa". Amesema alikataa kufanya utambuzi kulingana na hisia baada ya shambulio baya huko Rafah.

 

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo