Ukraine yapewa dola bilioni moja na Ubelgiji



Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy akizungumza wakati wa mkutano wa Baraza kuu la Usalama HUko New York . Picha na TIMOTHY A. CLARY / AFP.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy akizungumza wakati wa mkutano wa Baraza kuu la Usalama HUko New York . Picha na TIMOTHY A. CLARY / AFP.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy Jumanne alipokea ahadi ya pili ya dola bilioni moja ya msaada wa kijeshi kutoka Ubelgiji kwa ajili ya vita vinavyoendelea na Russia akiwa katika ziara yake barani Ulaya.

Jumatatu Zelenskyy alitia saini makubaliano ya ushirikiano na Uhispania ambayo itatenga dola bilioni moja nukta moja za msaada wa kijeshi kwa Ukraine mwaka huu, na dola bilioni tano nukta nne ifikapo mwaka 2027.

Msaada huo wa kati ya nchi mbili ulitangazwa wakati mawaziri wa ulinzi wa Umoja wa Ulaya wanakutana mjini Brussels kujaribu tena kusitisha pingamizi la Hungary la kutoa mabilioni ya euro kwa ajili ya msaada wa kijeshi kwa Kyiv, katika mwaka wake wa tatu wa vita tangu uvamizi wa Russia kuanza.

Akiwa mjini Brussels, Zelensky alimshutumu Rais wa Russia Vladimir Putin kwa kujaribu kuvuruga mkutano wa kilele wa amani wa Ukraine nchini Uswizi unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao.

"Tunawaomba viongozi wa dunia, kama mnataka amani, basi tukutane kwenye eneo la mkutano wa kilele wa amani. Ni hakika kabisa kwamba tunaandaa jukwaa hili pamoja na washirika wengine, kwa sababu vita ni yetu na juhudi ni zetu.sisi ni waathiriwa, tulivamiwa, tunauliwa na ndio sababu hamfai kuangalia sabbau zingine ila kufuata mkondo huu,” alisema rais huyo wa Ukraine.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo