Urusi yaonya Magharibi baada ya kusema kuwa Ukraine inaweza kushambulia Urusi kwa silaha zake

 .

Urusi imeishutumu Nato na Marekani kwa "kuchochea kiwango kipya cha mvutano" baada ya Marekani na Ujerumani kuwa washirika wa hivi punde kuruhusu jeshi la Ukraine kutumia silaha zinazotolewa na nchi za Magharibi kushambulia maeneo ndani ya Urusi.

Msemaji wa Berlin alisema Ujerumani ina imani kuwa Ukraine ina haki ya kujilinda dhidi ya Urusi, haswa kutokana na mashambulizi ya mpakani kwenye mji wake wa pili kwa ukubwa wa Kharkiv.

Maafisa wa Marekani walisema silaha zinazotolewa na Marekani zinaweza kutumika kukabiliana na Urusi karibu na eneo la Kharkiv, ama pale ambapo vikosi vya Urusi "vilikuwa vinawapiga au kujiandaa kuwapiga".

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema uamuzi huo utasaidia kuwalinda raia wanaoishi katika vijiji vilivyo karibu na mpaka wa Urusi.

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alisema nchi za Nato, hasa Marekani na nchi kadhaa za Ulaya, "zimeingia katika duru mpya ya mvutano unaozidi kuongezeka na wanafanya hivyo kwa makusudi", katika matamshi yaliyonukuliwa na shirika la habari la Tass.

"Kwa kila njia wanachochea Ukraine kuendeleza vita hivi vya kipumbavu."

Vikosi vya Urusi vimepata mafanikio katika eneo la Kharkiv katika wiki za hivi karibuni baada ya mashambulizi ya kushtukiza katika eneo hilo, karibu na mpaka na Urusi.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo