Usajili wa wagombea wa uchaguzi mapema wa rais wa Iran waanza


  • Usajili wa wagombea wa uchaguzi mapema wa rais wa Iran waanza

Iran leo imezindua mchakato wa siku tano wa usajili kwa watu wanaotarajia kugombea katika uchaguzi wa 14 wa rais kuchukua nafasi ya Ebrahim Raisi aliyekufa shahidi maisha katika ajali ya helikopta mapema mwezi huu.

Rais, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Hossein Amir-Abdollahian na wengine sita walikufa shahidi Mei 19, wakati helikopta yao ilipoanguka katika hali mbaya yaa hewa ya ukungu katika milima karibu na mpaka wa kaskazini-magharibi mwa nchi.

Wagombea wote lazima waidhinishwe na Baraza la Walinzi wa Katiba lenye  wanachama 12. Hicho ni chombo kikuu cha usimamizi wa uchaguzi nchini. Wizara ya Mambo ya Ndani itatangaza majina ya walioidhinishwa tarehe 11 Juni.

Kufuatia kufa shahidi Rais Rasi na wenzake, wakuu wa mihimili mitatu ya dola nchini Iran walikubaliana Jumatatu kwamba uchaguzi wa rais wa haraka utafanyika tarehe 28 Juni.

Kulingana na ratiba iliyotangazwa na serikali, kampeni zitaanza Juni 12 na zitaendelea hadi Juni 27.

Uchaguzi wa mapema wa urais unafanyika chini ya Vifungu vya 131 na 132 vya Katiba ya Iran ambavyo vinatamka kwamba rais mpya anafaa kuchaguliwa kwa kura za umma ndani ya muda usiozidi siku 50 kuanzia siku ambayo rais anakufa au kukosa uwezo.

Mnamo Mei 20, Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alimteua Makamu wa Rais Mohammad Mokhber kuchukua usimamizi wa tawi la mtendaji kulingana na Kifungu cha 131 cha Katiba.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China