Wapalestina 35 wachomwa moto wakiwa hai katika shambulio la kinyama la Israel Rafah

 

  • Wapalestina 35 wachomwa moto wakiwa hai katika shambulio la kinyama la Israel Rafah

Jeshi katili la utawala wa Kizayuni wa Israel limeshambulia kwa makombora kambi ya watu waliolazimika kuhama makazi yao na kuhamia eneo lililotengwa kuwa na usalama huko Rafah, na kuwaua shahidi Wapalestina 35, wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto.

Shambulio hilo la linyama la jeshi la Kizayuni katika eneo la Tal as-Sultan limefanywa wakati askari wa jeshi hilo wakishambulia pia kwa makombora makazi ya Wapalestina waliokimbia makazi yao katika maeneo ya Jabalia, Nuseirat na mji wa Ghaza na kuua watu wengine 160 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Hayo yanajiri huku Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Amnesty International likiitaka Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC ichunguze jinai na uhalifu wa kivita uliofanywa katika mashambulizi matatu ya hivi karibuni ya Israel yaliyoua raia 44 wa Palestina, wakiwemo watoto 32.

Jeshi la Kizayuni linavyoiteketeza Ghaza

Amnesty imesema mashambulizi hayo matatu yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel - moja kwenye kambi ya wakimbizi ya al-Maghazi katikati mwa Ghaza mnamo Aprili 16, na mawili huko Rafah kusini mwa Ghaza mnamo Aprili 19 na 20 - "ni ushahidi zaidi wa muundo mpana wa uhalifu wa kivita" uliofanywa na Israel katika Ukanda wa Ghaza.

Akiashiria mashambulio hayo ya kinyama, Mkurugenzi Mwandamizi wa Amnesty International Erika Guevara-Rosas amesema: "kesi zilizoorodheshwa hapa zinaonyesha mfano wa wazi wa mashambulizi yaliyofanywa katika kipindi cha miezi saba iliyopita ambapo jeshi la Israel limekiuka sheria za kimataifa, na kuua raia wa Palestina bila kuadhibiwa kabisa na kuonyesha kutojali maisha ya binadamu".

Wapalestina wapatao 35,984 wameshauawa shahidi hadi sasa na wengine 80,643 wamejeruhiwa tangu utawala wa Kizayuni ulipoanzisha vita vya kinyama vya mauaji ya kimbari dhidi ya Ghaza mnamo Oktoba 7, 2023.../

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China