Yemen yaapa kutoa jibu la 'kuumiza mno' baada ya shambulio la US na UK kuua makumi ya watu
Yemen imeapa kuwa itatoa jibu la "kuumiza mno" kwa mashambulizi yaliyofanywa na Marekani na Uingereza dhidi ya meneo kadhaa ya taifa hilo la Kiislamu, na kusababisha vifo vya watu wapatao 16 na kuwajeruhi wengine kadhaa.
Ali al-Qahoum, mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya harakati ya
Muqawama ya Ansarullah ya Yemen, ameiambia televisheni ya al-Mayadeen ya
Lebanon: "ni hakika kabisa kwamba Yemen itajibu vitendo vya kichokozi
vya Marekani na Uingereza dhidi ya nchi yetu; na muungano wa Marekani na
Uingereza hautaweza kuzuia majibu yetu".
Al-Qahoum amebainisha kwa kusema: "Wamarekani na Waingereza lazima
wawe wameelewa jinsi mashambulio ya Yemen yatavyokuwa makali. Makombora
yetu ya balestiki yanaweza kulenga shabaha tunazotaka baharini na katika
maeneo ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu".
Afisa huyo wa Ansarullah ameeleza kuwa Marekani ambayo ni mshirika mkuu wa Israel na muungaji mkono wa uvamizi unaendelea kufanywa na utawala huo ghasibu katika Ukanda wa Ghaza, haina nia yoyote ya kuzuia mgogoro usisambae katika eneo.
Amsema, kama Marekani haina nia ya kupanua wigo wa vita, inapaswa
ikomeshe uungaji mkono wake kwa uvamizi wa Israel dhidi ya Ghaza na
mzingiro ilioliwekea eneo hilo. Bila ya hivyo, mashambulizi ya Yemen
yataendelea, na wigo wake pia utapanuka.../