Al Houthi: Jeshi la Yemen litaendelea kushambulia manowari kubwa ya kivita ya Marekani

 

  • Al Houthi: Jeshi la Yemen litaendelea kushambulia manowari kubwa ya kivita ya Marekani

Kiongozi wa Harakati ya Muqawama ya Ansarullah ya Yemen ameapa kwamba Jeshi la nchi hiyo litaendelea kulenga meli kubwa ya kivita ya Marekani yenye uwezo wa kusheheni ndege za kivita ijulikanayo kama USS Dwight D. Eisenhower.

Hadi sasa Jeshi la Yemen limeishambulia manowari hiyo ya kisasa ya Marekani mara mbili katika operesheni za kujibu uchokozi wa Marekani dhidi ya Yemen na pia kuwaunga mkono Wapalestina wa Ukanda wa Gaza ambao wanakabiliwa na mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na Israel kwa himaya kamili ya Marekani.

Abdul-Malik al-Houthi alisema katika hotuba yake siku ya Alhamisi kwamba "Manowari ya Marekani yenye kusheheni ndege za kivita, 'Eisenhower' itasalia kuwa shabaha ya wanajeshi wa Yemen wakati wowote fursa inapotokea,".

Manoari hiyo ililengwa na vikosi vya Yemen katika Bahari ya Sham siku ya Ijumaa na kisha Jumamosi.

Vikosi vya Marekani na Uingereza vimekuwa vikifanya mashambulizi mbalimbali dhidi ya Yemen kama njia ya kujaribu kusitisha operesheni zake zinazoiunga mkono Palestina.

Hivi karibuni, ndege za kivita za Marekani na Uingereza zililenga majimbo ya magharibi mwa Yemen ya Sana'a, al-Hudaydah na Ta'izz, na kuua watu wasiopungua 16 na kujeruhi wengine zaidi ya 40.

Al Houthi alisema baada ya mashambulio ya vikosi vya Yemen, "meli hiyo ya kivita ya Marekani yenye kusheheni ndege ilisonga mbali kutoka pwani ya Yemen.  Kiongozi wa Ansarullah amesema 'Eisenhower' ilikuwa kilomita 400 kutoka pwani ya Yemeni wakati ilipolengwa, kisha ikahamia takriban kilomita 880 kaskazini magharibi mwa wa Jeddah."

Washington, hata hivyo, ilijaribu kukanusha kwamba meli hiyo ilikuwa ikilengwa, al-Houthi aliongeza, na kusema sababu ya kukanusha huko ni kuepuka fedheha.

Jeshi la Yemen limefanya mashambulizi mengi yanayoiunga mkono Palestina tangu Oktoba 7, wakati utawala wa Israel ulipoanzisha vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China