Bagheri: Operesheni ya Ahadi ya Kweli ilitokomeza uwezo bandia wa Israel wa kuzuia hujuma

 

  • Bagheri: Operesheni ya Ahadi ya Kweli ilitokomeza uwezo bandia wa Israel wa kuzuia hujuma

Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: "ubunifu na uamuzi wa Iran wa kumtia adabu mchokozi kwa operesheni ya Ahadi ya Kweli umetokomeza na kufuta uwezo hewa na bandia wa kuzuia hujuma na mashambulio wa utawala wa Kizayuni".

Ali Bagheri ameeleza hayo katika mkutano wa kimataifa uliofanyika leo hapa mjini Tehran kwa anuani: "Ghaza; Mdhulumiwa Aliye Imara", ambapo mbali na kusisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaendelea kuunga mkono harakati za Muqawama katika eneo amesema: leo hii, Ghaza iliyo imara na inayodhulumiwa ndiyo suala muhimu zaidi kwa ulimwengu.

Bagheri amesema, Muqawama wa Kiislamu si vuguvugu la kisiasa au kijamii, bali ni suala ambalo chimbuko lake limo ndani ya imani na itikadi ya wananchi wa Palestina na watetezi wa uhuru duniani na akaongeza kuwa: Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa ilikuwa hatua ya mabadiliko makubwa katika historia ya Palestina na kwa muelekeo wa uwepo haramu wa utawala wa Kizayuni, na hivi sasa utawala huo ndicho kitu kinachochukiwa zaidi katika sayari ya dunia.

Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameeleza bayana kuwa, utawala wa Kizayuni na waungaji mkono wake wa Magharibi inawapasa wajue kwamba hawana njia nyingine isipokuwa kukubali mazungumzo na akaongeza kuwa: leo hii Muqawama wa Ghaza uko imara zaidi kuliko ulivyokuwa hapo kabla, na huo ni ujumbe mzito kwa Wazayuni.

Naye Mohammad Baqher Qalibaf, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekumbusha katika hotuba yake kwa mkutano huo kwamba Imam Khomeini (MA) aliichukulia Palestina kuwa ndio suala na mhimili mkuu na utatuzi wa suala hilo ni kuangamizwa utawala wa Kizayuni na akasema: Iran siku zote imekuwa bega kwa bega na watu wa Palestina na inaitakidi kuwa taifa hili lenyewe ndilo linalopaswa kujiamulia mustakabali wake.

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema: unyama unaofanywa na Israel ni mjibizo unaotokana na hofu ya kutoweza kuendelea kubaki, na hakuna yeyote anayeelewa barabara zaidi kuliko Israel yenyewe kwamba wimbi hili la Muqawama ambalo mhimili wake mkuu ni Wapalestina wenyewe ama leo au kesho litaing'oa mizizi ya dude hilo la nuhusi.../

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China