Chama cha ANC chatafuta washirika kuunda serikali

 


  • Chama cha ANC chatafuta washirika kuunda serikali

Chama tawala cha Afrika ya Kusini cha African National Congress (ANC) kiko njiapanda katika juhudi zake za kusaka washirika kinachoweza kuunda nao serikali ya pamoja.

Chama hicho kinakabiliwa na changamoto hiyo baada ya kupoteza wingi wa viti vya bunge katika uchaguzi uliofanyika wiki iliyopita ikiwa ni mara ya kwanza tangu kilipoingia madarakani nchini Afrika Kusini miaka 30 iliyopita.

Vyama vyenye uwezekano wa kuunda ushirika na chama cha ANC vyenye itikadi tofauti zinazokinzana ni pamoja na Democratic Alliance, chama cha aliyekuwa Rais wa zamani Jacob Zuma cha uMkhonto we Sizwe pamoja Economic Freedom Fighters (EFF) cha Julius Malema.

Chama cha DA na chama kidogo cha  Inkatha Freedom (IFP) vilishatangaza kuwa vimeandaa timu za wawakilishi wao kwa ajili ya majadiliano na vyama vingine. Vyama hivyo ni sehemu ya muungano ulioanzishwa kabla ya uchaguzi.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa 

 

Kulingana na katiba ya Afrika ya Kusini, bunge jipya lililotokana na uchaguzi huo linapaswa kuanza kazi ndani ya wiki mbili baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi na moja ya majukumu yake ya awali ni kumchagua Rais ajaye wa taifa hilo.

KKwa mujibu wa nmatokeo ya uchaguzi Chama cha ANC kimeshinda chini ya nusu ya viti katika Bunge la Afrika Kusini kwa kupata viti 159 kati ya 400. Katika bunge lililopita, ANC ilikuwa na viti 230.

Chama cha Democratic Alliance (DA) - chama kilichoshika nafasi ya pili katika uchaguzi - kimeteua timu ya mazungumzo wakati kikianza mazungumzo ya kuunda muungano na ANC.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo