HAMAS yatoa pigo jingine angamizi dhidi ya wanajeshi wa Israel

 


  • HAMAS yatoa pigo jingine angamizi dhidi ya wanajeshi wa Israel

Brigedi za Shahid Izzuddin al Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS zimetoa pigo jingine kubwa kwa wanajeshi vamizi wa Israel katika mji wa Rafah wa kusini mwa Ukanda wa Ghaza.

Jana Jumatatu, wanamapambano wa HAMAS waliweka mtego wa jengo lililotegwa mabomu katika kambi ya wakimbizi ya al Shabura huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Ghaza na kuangamiza wanajeshi wengi wa Israel.

Kanali ya televisheni ya al Mayadeen imesema katika ripoti yake kwamba jeshi la utawala wa Kizayuni lilitumia helikopta kuzoa maiti na majeruhi wake walioangamizwa na HAMAS baada ya kuingia kwenye jengo la ghorofa na kuripuliwa kwa mabomu yaliyokuwa yametegwa humo na harakati hiyo ya Kiislamu.

Ijapokuwa utawala wa Kizayuni unachuja mno habari, lakini pamoja na hayo, vyombo vya habari vya Israel vimekiri kwamba wanajeshi wanne wa utawala huo wameangamizwa na wengine 10 wamejeruhiwa, huku sita kati yao wakiwa katika hali mahututi. 

Miezi minane sasa utawala wa Kizayuni unafanya jinai za kutisha dhidi ya wananchi wa Palestina lakini kutokana na mapambano ya kishujaa na muqawama wa kupigiwa mfano wa wananchi hao, wanajeshi makatili wa Israel wameshindwa kufanikisha hata lengo moja la kuanzisha vita hivyo zaidi ya kufanya jinai za kuogofya dhidi ya wanawake na raia wa kawaida hasa wa Ghaza.

Tags




Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China