Haniya: HAMAS haitasalimu amri, itaendeleza muqawama

 


  • Haniya: HAMAS haitasalimu amri, itaendeleza muqawama

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kundi hilo la muqawama katu halitasalimu amri, bali litaendeleza mapambano yake kwa nguvu zote.

Ismail Haniya amesema hayo katika taarifa, akijibu operesheni ya umwagaji damu iliyofanywa na wanajeshi makatili wa Israel dhidi ya kambi ya wakimbiizi ya Nuseirat, katikati mwa Ukanda wa Gaza na kuongeza kuwa: Hatutakata tamaa, tutaendelea kupigania haki zetu za msingi mkabala wa adui mtenda jinai.

Wapalestina wasiopungua 210 waliuliwa shahidi na wengine zaidi ya 400 walijeruhiwa juzi Jumamosi katika mashambulizi ya kinyama ya anga ya Israel yaliyolenga kambi ya wakimbizi ya Nuseirat, maeneo ya mashariki ya Deir al-Balah, na kambi za al-Bureij na al-Maghazi katikati mwa Gaza, sanjari na uvamizi wa ghafla uliofanywa na magari mashariki na kaskazini magharibi mwa Nuseirat.

Jinai za Wazayuni katika kambi ya Nuseirat

Haniya amesema katika taarifa kuwa, "Wazayuni watenda jinai wanadhani kwamba kwa kuwalenga watoto na wanawake kambini watavunja azma ya Wapalestina, lakini umwagaji damu huu utaimarisha tu uthabiti wetu katika misingi yetu na kushikamana kwetu na ardhi yetu."

Brigedi za Izzuddin Qassam, Tawi la Kijeshi la HAMAS zimeendelea kuzipiga kwa makombora ngome za utawala wa Kizayuni katika maeneo tofauti ya Ukanda wa Gaza.

HAMAS inasisitiza kuwa, mashambulizi yote hayo ni katika kujibu jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina hasa wa Ukanda wa Gaza.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China