Harakati ya Kiislamu ya Iraq yatelekeza mashambulizi mapya dhidi ya Israel
Katika kukabiliana na hujuma za utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza hususan katika mpaka wa kusini mwa mji wa Rafah, wapiganaji wa Harakati ya Kiislamu ya Iraq wamefanya operesheni mbili tofauti dhidi ya mitambo ya kimkakati ya ardhi za Palestina zilizokaliwa kwa mabavu mwaka 1948 na kupachikwa jina bandia la Israel
Katika kukabiliana na hujuma za utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza hususan katika mpaka wa kusini mwa mji wa Rafah, wapiganaji wa Harakati ya Kiislamu ya Iraq wamefanya operesheni mbili tofauti dhidi ya mitambo ya kimkakati ya ardhi za Palestina zilizokaliwa kwa mabavu mwaka 1948 na kupachikwa jina bandia la Israel.
Harakati ya Mapambaano ya Kiislamu ya Iraq lilisema kwenye tangazo lake mtandaoni kwamba wapiganaji wake walifanya shambulio la ndege zisizo na rubani dhidi ya kiwanda cha kusafisha mafuta katika mji wa bandari wa Haifa. Taarifa hiyo imesisitiza kwamba shambulio hilo liligonga malengo yaliyowekwa kwa usahihi.
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Iraq ambayo ni kundi mwavuli la vikundi vya kupambana na ugaidi nchini Iraq imebaini kwamba pia imetekeleza operesheni tofauti dhidi ya maeneo "muhimu" kwenye Bandari ya Haifa kwa kutumia ndege za kivita zisizo na rubani.
Mapema Jumapili, Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Iraq ilisema katika taarifa iliyochapishwa kwenye kanali yake ya Telegram kwamba, ilifanya shambulio la ndege isiyo na rubani kwenye eneo lililolengwa na Israel katika Bandari ya Eilat katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.
Muungano huo umekuwa ukifanya mashambulizi kadhaa dhidi ya Israel tangu utawala huo ghasibu uanzishe vita vya mauaji ya halaiki huko Gaza mapema mwezi Oktoba.
Takriban Wapalestina 36,439 wameuawa, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na watu wengine 82,627 wamepata majeraha tangu Israel ianzisha vita dhidi ya Gaza zaidi ya miezi minane iliyopita.