Hizbullah: Kama Israel inataka kuingia kwenye vita kamili, sisi tuko tayari kwa hilo
Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema: "sisi tuko tayari kwa vita kamili na vya pande zote na utawala wa Kizayuni".
Kwa mujibu wa IRNA, Sheikh Naim Qassem, amesisitiza kuwa:
hatua yoyote ya Israel ya kupanua vita na Lebanon itasababisha
maangamizi na uharibifu kwa utawala huo na kwa Wazayuni kulazimika
kuyahama makazi yao katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.
Naim Qassem amebainisha kwa kusema: "katika kipindi cha miezi
miwili iliyopita, tulipewa vitisho mara kadhaa kututaka tuache kupigana
vita na Wazayuni, lakini jibu letu lilikuwa ni kwamba kambi ya Lebanon
imeungana na kambi ya Ukanda wa Ghaza".
Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameeleza pia kuwa: kwa
kuzingatia aina ya sasa ya vita inavyopigana na jeshi la Israel,
Hizbullah imetumia sehemu ndogo tu ya uwezo wake.
Kuhusu mpango uliopendekezwa na Rais Joe Biden wa Marekani wa kusitisha mapigano katika Ukanda wa Ghaza na kubadilishana mateka, Sheikh Naim Qassem amesema: mapendekezo ya Biden ya kutuliza hali ya mambo hayana maana; na mpango wake ni kwa ajili ya uchaguzi wa hivi sasa nchini Marekani.
Ijumaa ya Mei 31, Rais Joe Biden wa Marekani alidai kwamba utawala
wa Kizayuni umewasilisha pendekezo jipya la usitishaji vita na
kubadilishana mateka na akazitaka pande husika kutopoteza fursa hiyo na
kufikia makubaliano juu ya pendekezo hilo; pendekezo ambalo linajumuisha
pia kuachiliwa mateka wa Kizayuni na kujengwa upya kwa Ukanda wa Ghaza.
Katika miezi michache iliyopita na kufuatia jinai za kutisha za
utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza na mauaji ya kimbari
uliyofanya dhidi ya Wapalestina katika eneo hilo, Hizbullah ya Lebanon
imezishambulia ngome za kijeshi ya utawala huo kaskazini mwa ardhi
zinazokaliwa kwa mabavu, suala ambalo limezua hofu kubwa kwa walowezi wa
Kizayuni wanaoishi katika maeneo hayo.
Hadi sasa makumi ya maelfu ya Wazayuni wamevihama vitongoji
vilivyoko karibu na mipaka ya Lebanon kwa kuhofia mashambulizi ya
Muqawama.../