Hizbullah ya Lebanon yadungua ndege isiyo na rubani ya utawala wa Kizayuni
Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Lebanon Hizbullah imeidungua ndege isiyo na rubani ya jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel ndani ya anga ya Lebanon.
Utawala wa Kizayuni hukiuka anga ya Lebanon kila mara na kushambulia maeneo tofauti ya nchi hiyo.
Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
IRIB, Hizbullah ya Lebanon imetangaza kuwa vikosi vya harakati hiyo ya
Muqawama vimeiangusha ndege isiyo na rubani ya utawala wa Kizayuni aina
ya Hermes 900 katika anga ya Lebanon.
Jeshi la utawala wa Kizayuni limekiri kwamba ndege yake moja isiyo
na rubani iliyokuwa ikiruka katika anga ya kusini mwa Lebanon
imedunguliwa kwa kombora la kutoka ardhini kuelekea angani.
Karibu wiki mbili zilizopita Hizbullah ya Lebanon iliteketeza puto la kisasa zaidi kiteknolojia na la gharama kubwa zaidi la ujasusi la Israel katika shambulio la ndege isiyo na rubani ililofanya kwa kuvuka matabaka tata ya ulinzi wa anga ya utawala wa Kizayuni.
Kwa miezi kadhaa sasa, na kufuatia jinai za kutisha za utawala wa
Kizayuni na mauaji ya kimbari unayofanya dhidi ya Wapalestina wa Ukanda
wa Ghaza, Hizbullah ya Lebanon imekuwa ikiyalenga maeneo ya kijeshi ya
Wazayuni kaskazini mwa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu, suala ambalo
limewafanya walowezi wa Kizayuni wanaoishi katika maeneo hayo kuingiwa
na hofu kubwa, ambapo hadi sasa makumi ya maelfu ya Wazayuni hao
wameondoka katika vitongoji vilivyoko karibu na mpaka wa Lebanon kwa
kuhofia mashambulizi ya Muqawama.../