Jeshi la wanamaji la Urusi kukuzwa na meli mpya zaidi ya 40 - Putin

 Jeshi la wanamaji la Urusi kukuzwa na meli mpya zaidi ya 40 - Putin

Vladimir Putin anasema jeshi la wanamaji la Urusi litaimarishwa na angalau meli mpya 40 mnamo 2024.

Katika ripoti ya shirika la habari la serikali TASS, kiongozi huyo wa Urusi amenukuliwa akisema kuwa moja ya malengo makuu ya nchi hiyo ni "kuboresha kikamilifu" uwezo wake wa majini.

Hii inajumuisha "meli, ndege na sehemu za pwani", wakati pia kuna mipango ya kuboresha miundombinu ya besi za majini ili "kuimarisha nafasi zake katika maeneo muhimu ya kimkakati ya bahari ya dunia, na kuboresha kwa kiasi kikubwa uwezo wake wa kupambana".

Bw Putin alisema, ikilinganishwa na miaka ya nyuma ambapo idadi ilikuwa chini, 2024 ingeshuhudia meli na boti zaidi ya 40 zikipokelewa.

"Mengi yamefanywa katika eneo hili, kwani Jeshi letu la Wanamaji linapata meli mpya," alisema, na kuongeza kuwa "matengenezo na urekebishaji wa kina wa vifaa" unafanywa.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo