Jihadul-Islami: Tunautazama mpango uliopendekezwa na Biden kwa 'jicho la shaka'
Harakati ya Muqawama ya Jihadul-Islami ya Palestina imesema inautazama kwa jicho la shaka mpango uliotangazwa na Rais wa Marekani kwa ajili ya kuhitimisha vita vya Ghaza.
Taarifa iliyotolewa na Jihadul-Islami kubainisha msimamo wake
juu ya mpango uliotangazwa jana na Rais Joe Biden wa Marekani kwa ajili
ya kuhitimisha vita vya Ghaza imeeleza kuwa, harakati hiyo inalitazama
kwa jicho la shaka pendekezo la rais wa Marekani linalojaribu kuonyesha
kwamba serikali ya Marekani imebadilisha msimamo wake.
Harakati hiyo ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina imesema:
"ingali ni wazi kuwa serikali ya Marekani inaupendelea kikamilifu
utawala wa Kizayuni, inaficha jinai zake na inashiriki katika uchokozi
unaofanya".
Taarifa ya Jihadul-Islami imeendelea kueleza: "tutatathmini pendekezo lolote lile kwa njia ambayo itahakikisha kunakomeshwa vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya watu wetu, kulindwa maslahi na haki zao, na kukidhi matakwa ya Muqawama".
Sehemu nyingine ya taarifa hiyo imesema, Jihadul-Islami inalitalii
pendekezo la rais wa Marekani na kuchukua msimamo wa kitaifa kuhakikisha
uvamizi unakomeshwa; na jeshi la Kizayni linaondoka kikamlifu Ukanda wa
Ghaza.../