Kundi la kwanza la askari wa Ufaransa liko njiani kuelekea Ukraine


  • Kundi la kwanza la askari wa Ufaransa liko njiani kuelekea Ukraine

Mbunge wa Ukraine Aleksey Goncharenko amesema kundi la kwanza la wakufunzi wa kijeshi wa Ufaransa liko njiani kuelekea nchini humo.

Haya yanajiri siku chache baada ya kamanda mkuu wa Ukraine, Aleksandr Syrsky, kutangaza kuwa ameidhinisha kuwepo kwa askari wa Ufaransa nchini humo.
 
Goncharenko, ambaye ni mbunge wa bunge la Ukraine na mjumbe wa Baraza la Bunge la Baraza la Ulaya, ameandika kwenye mtandao wa X: "vyanzo vyangu vimenifahamisha kwamba kundi la kwanza la wakufunzi wa Ufaransa tayari liko njiani kuelekea Ukraine".
 
Itakumbukwa kuwa, mnamo mwezi Februari, Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa alisema hawezi kuondoa uwezekano wa nchi wanachama wa shirika la kijeshi la Magharibi NATO kutuma wanajeshi Ukraine katika siku zijazo, ingawa maafisa wa Ufaransa walifafanua hivi karibuni kwamba alimaanisha askari wasio wapiganaji. Macron baadaye alisema kwamba NATO inapaswa kupitisha sera ya "utata wa kimkakati" kuhusiana na Russia.
Putin (kushoto) na Biden

Bloomberg iliripoti jana kuwa, kiongozi huyo wa Ufaransa amekuwa akifanya kazi nyuma ya pazia kuunda muungano wa nchi zilizo tayari kupeleka wakufunzi wa kijeshi huko Kiev.

 
Hayo yanajiri huku Moscow ikiwa imeshaonya kwamba msaada wowote wa ziada wa kijeshi kwa Kiev utashadidisha vita.
 
Siku ya Jumanne, Rais Vladimir Putin wa Russia alivieleza vyombo vya habari kuwa wanajeshi wa Magharibi tayari wanafanya kazi nchini Ukraine na akafafanua kwa kusema: "wamekuwa huko kwa muda mrefu, wao ni wataalamu [wa kigeni] chini ya kivuli cha mamluki".
Putin alitoa indhari kwamba kutumwa vikosi vya majeshi ya Magharibi nchini Ukraine itakuwa "hatua nyingine ya kuelekea mzozo mkubwa wa Ulaya na wa ulimwengu mzima".../

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo