Mafanikio ya kihistoria ya kudumu ya Shahid Raisi aliyekufa shahidi na wenzake, katika sekta ya mafuta na gesi


  • Mafanikio ya kihistoria ya kudumu ya Shahid Raisi aliyekufa shahidi na wenzake, katika sekta ya mafuta na gesi

Tangu kuingia madarakani serikali ya awamu ya 13, miradi mikubwa 132 ambayo ilikuwa haijakamilika yenye thamani ya dola bilioni 28.5 imekamilika katika sekta ya mafuta na gesi, na wakati huo huo kuanza utekelezaji wa miradi mipya 50 yenye thamani ya dola bilioni 47.5.

Kufuatia kidiplomasia hai ya serikali ya 13 katika kuendeleza uhusiano na nchi tofauti na sio za Ulaya na Marekani pekee, uzalishaji na uuzaji nje mafuta ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ulianza mwenendo unaokua tangu mwaka 2021 ambapo hivi sasa Iran inauza nje mapipa milioni 1.5 ya mafuta kwa siku.

Katika umri wake wa siku 1000 serikali ya awamu ya 13 imeweza kuongeza uzalishaji wa mafuta kwa asilimia 63 kwa siku ambapo kufuatia juhudi zake kubwa za kutafuta masoko na kuimarisha kidiplomasia ya nishati, imeweza kuandaa uwanja mzuri wa kushirikiana na nchi nyingine katika nyanja za mafuta, uuzaji mafuta, bidhaa za mafuta, bidhaa za petrochemical na hivyo kuongeza kiwango cha mauzo ya mafuta ghafi kwa asilimia 40 na kupata mapato ya dola bilioni 36.

Mafanikio ya kudumu ya Shahid Rais Raisi aliyekufa shahidi katika ajali ya helikopta

Moja ya sifa muhimu za serikali ya marehemu Shahid Rais Raisi ni kutokutegemea mazungumzo na kuondolewa vikwazo vya kimataifa kwa ajili ya maendeleo kwani serikali ya awamu ya 13 imepata maendeleo makubwa katika sekta ya nishati hususan mafuta na gesi kwa kutegemea mashirika ya ndani na diplomasia hai. Mafanikio haya yote yamepatikana katika hali ambayo hisa ya mashirika ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika uendeshaji wa miradi ya mafuta na gesi katika miaka ya mwanzo ya miradi ya ustawi wa Pars Kusini ilikuwa chini ya asimia 30.

Kukamilishwa miradi ambayo ilikuwa haijakamilika katika sekta ya mafuta katika kipindi cha miezi 33 iliyopita kumepelekea ongezeko la asilimia 63 ya uzalishaji wa mafuta ghafi na asilimia 6 katika uzalishaji wa gesi. Pia, uwezo wa kusafisha mafuta ghafi uliongezeka kutoka mapipa milioni 2,100 kwa siku hadi mapipa milioni 2,370 na uzalishaji wa bidhaa za petrokemikali kutoka tani milioni 60 kwa mwaka hadi tani milioni 75, ambalo ni  ongezeko la asilimia 16.
Miongoni mwa miradi iliyokamilishwa tangu kuanza kazi serikali ya awamu ya 13 hadi May tarehe 21,2024 mwaka huu, ni kukamilishwa na kuzinduliwa awamu ya kwanza ya mradi wa maendeleo wa visima vya mafuta vya Sepehr na Jafir kwa uwekezaji wa dola bilioni 2.8.

Kukamilika na uendeshaji wa miradi hii umeongeza uwezo wa uzalishaji mafuta kwa zaidi ya mapipa 160,000 kwa siku. Hali kadhalika kutiwa saini mikataba mipya ya kuongeza uwezo wa uzalishaji wa mafuta ghafi kunatabiri kuendeleza hali ya sasa ya kukua uchumi.

Hatua ya serikali ya Shahid Raisi ya kuunda kitovu cha gesi kieneo nchini Iran

Kuzinduliwa miradi hii kunaweza kuongeza uwezo wa uzalishaji wa mafuta ghafi kwa mapipa 650,000 kwa siku. Pamoja na kukamilishwa miradi ambayo haijakamilika na kuhitimisha kandarasi mpya katika sekta ya mafuta, hatua nzuri pia zimechukuliwa kwa ajili ya kutekeleza miradi mipya katika sekta hiyo. Uwekezaji wa zaidi ya dola bilioni 26 umepangwa kuongeza uwezo wa uzalishaji wa gesi hadi mita za ujazo milioni 260 kwa siku.

Uwekezaji mkubwa wa dola bilioni 3.5 pia umefanyika katika uwanja wa kuongeza uwezo wa kuzalisha bidhaa za petrokemikali ambapo jambo hilo limeongeza uzalishaji huo kwa tani milioni 10.

Serikali ya awamu ya 13 ya Shahidi Ayatollah Shahid Rais Raisi pia imechukua hatua chanya katika uga wa kukamilisha miradi ya mabomba ya kitaifa ya kusambaza gesi na bidhaa za mafuta.
Miongoni mwa miradi hiyo tunaweza kutaja kukamilika na kuzinduliwa bomba la kusafirisha mafuta lenye urefu wa zaidi ya kilomita 1,000 lenye ujazo wa mapipa 665,000 kwa siku kwa uwekezaji wa dola bilioni 1.2 na kilomita 1,800 za bomba la kitaifa la kusafirisha gesi kwa uwekezaji wa dola bilioni 1.5.

Serikali ya awamu ya 13 ya Shahid Raisi haijasimamisha maendeleo ya nchi na kusibiri kufikiwa makubaliano na Marekani na nchi za Ulaya, bali imeanda fursa mpya za maendeleo ya nchi kwa kupunguza mivutano na kuimarisha uhusiano na nchi za eneo pamoja na  kujiunga na jumuiya muhimu kimataifa zikiwemo za Shanghai na BRICS.

Wakati huo huo serikali ya awamu ya 13 haijasimamisha mazungumzo na Marekani na nchi za Ulaya ambapo mazungumzo hayo yanaendelea kwa njia ya kuheshimiana pande zinazoshiriki mazungumzo na bila shaka kufikiwa matokeo yanayotarajiwa kutaiandalia Jamhuri ya Kiislamu ya Iran fursa nyingine ya kunyanyua hadhi yake.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China