Makaburi ya halaiki na mifuko ya kubeba miili ndio inayopatika al-Shifa baada ya Israel kuondoa majeshi yake

 .

Baada ya wanajeshi wa Israel kuondoka katika jengo kubwa la hospitali ya al-Shifa katika mji wa Gaza tarehe 1 mwezi Aprili, kufuatia uvamizi wao wa pili hapo, Wapalestina walishtushwa na waliokuwa wakitafuta magofu yaliyoteketea wakisema ni watu waliouawa.

Katika kipindi cha miezi minane ya vita, hospitali zimekuwa zikishambuliwa mara kwa mara, huku Israel ikidai kuwa zinatumiwa kama vituo na Hamas; kitu ambacho kundi hilo linakanusha.

Lakini matukio ya al-Shifa - ambayo zamani ilikuwa kituo kikubwa cha matibabu na chenye vifaa bora zaidi katika Ukanda wa Gaza - bila shaka yamekuwa ya kushangaza zaidi.

Uvamizi huo wa kushtukiza wa wiki mbili, ulioanzishwa baada ya Israel kusema kuwa Hamas wamejipanga upya katika eneo hilo, ulielezwa na serikali ya Israel kama "sahihi na ni upasuaji".

Msemaji wake, Avi Hyman, alisema: "Tuliondoa zaidi ya magaidi 200. Tuliwakamata magaidi zaidi ya 900 bila hata raia mmoja kujeruhiwa.”

Huku miili iliyooza ikitolewa nje ya mchanga iliyorundikwa na tingatinga katika ua wa al-Shifa, madai kwamba hakukuwa na raia waliojeruhiwa yalitiliwa shaka papo hapo.

Katika wiki za hivi karibuni, makaburi manne ya halaiki yamegunduliwa katika eneo hilo, huku timu za watafutaji wa Palestina zikisema kuwa mamia ya maiti zimepatikana.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo