'Mimi ni mtesaji wa wabaguzi wa rangi' - Vinicius jr

.

Mshambulizi wa Real Madrid, Vinicius Jr anasema ni "mtesaji wa wabaguzi wa rangi" baada ya mashabiki watatu wa Valencia kuhukumiwa kifungo cha miezi minane jela kwa kosa la kumtusi kwenye mechi.

Nyimbo zao za kibaguzi zilimlenga Vinicius wakati wa mchezo wa La Liga kwenye Uwanja wa Mestalla huko Valencia mnamo Mei 21, 2023.

Mashabiki hao walipatikana na hatia ya "uhalifu dhidi ya uadilifu wa maadili" na "hali inayozidisha ubaguzi kulingana na nia za kibaguzi".

"Mimi si mwathirika wa ubaguzi wa rangi. Mimi ni mtesaji wa wabaguzi wa rangi. Hukumu hii ya kwanza ya uhalifu katika historia ya Uhispania sio yangu. Ni ya watu wote weusi," Vinicius alichapisha kwenye X.

"Wabaguzi wengine waogope, waaibike na wajifiche kwenye vivuli. Vinginevyo, nitakuwa hapa kukusanya. Asante kwa La Liga na Real Madrid kwa kusaidia na hukumu hii ya kihistoria."

Ni mara ya kwanza kwa hukumu ya ubaguzi wa rangi katika mechi ya soka nchini Uhispania kutolewa na ilikuwa ni matokeo ya moja kwa moja ya malalamiko yaliyowasilishwa na La Liga.

Hukumu ya awali ya miezi 12 ilipunguzwa kwa theluthi kufuatia makubaliano yaliyoafikiwa katika hatua ya awali ya uchunguzi.

Mashabiki hao pia walipigwa marufuku kuingia katika uwanja wowote wa soka ambamo mechi za La Liga na/au Shirikisho la Soka la Uhispania (RFEF) huchezwa kwa kipindi cha miaka mitatu, baadaye kupunguzwa hadi miwili.

Mchezaji wa kimataifa wa Brazil Vinicius alijiunga na La Liga, Real Madrid na RFEF katika kupeleka kesi hiyo mahakamani. Washtakiwa walisoma barua ya kuomba radhi wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo.

Rais wa La Liga, Javier Tebas alisema: "Uamuzi huu ni habari njema kwa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Uhispania, kwani huenda kwa njia fulani kurekebisha makosa ya aibu aliyotendwa Vinicius Jr na kutuma ujumbe wazi kwa watu wanaoenda kucheza mpira.

“La Liga itawatambua, itawaripoti, na kutakuwa na matokeo ya uhalifu.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China