Modi yuko tayari kwa muhula wa tatu lakini upinzani bado haujakubali
Matokeo rasmi yanaonyesha muungano unaoongozwa na Waziri Mkuu Narendra Modi nchini India umeshinda viti vya kutosha kuunda serikali ijayo.
Lakini chama chake cha BJP kimeshindwa kupata wingi wa viti peke yake, na kushinda viti vichache sana kuliko katika uchaguzi uliopita.
Waziri Mkuu Narendra Modi alihutubia wafuasi wake Jumanne, akisema: "Ushindi wa leo ni mkubwa zaidi ulimwenguni".
Alieleza kuwa ni "ushindi kwa Wahindi".
Aliapa kwamba hatakoma hadi umaskini utakapomalizika "kabisa" nchini humo.
Pia aliapa kutokomeza rushwa na kuondokana na makaa ya mawe hadi “vyanzo vya nishati mbadala”.
Modi alimalizia kwa kusema "ishi maisha marefu nchi yangu India!"